Friday, June 1, 2012
LEO KIPINDI CHA CHA XXL KINACHORUSHWA NA CLOUDS FM KILIRUKA LIVE CLODS TV AMBAPO WASANII TOFAUTI WALISHIRIKI KWENYE SHOO HIYO.
XXL CREW,wakwanza aliyevaa miwani ya rangi nyeusi ni B DAZEN,wa pili ni BABA JOHNII,watatu mschana ni MWANADADA D na Cameraman RAY.
BAADHI YA WAREMBO WATAKAOPANDA JUKWAANI KATIKA SHINDANO LA MISS NYAMAGANA JIJINI MWANZA LEO
Aisha.
HIZI NI BAADHI YA SURA ZITAKAZOPANDA JUKWAANI USIKU WA LEO IJUMAA, KATIKA SHINDANO LA MISS NYAMAGANA 2012. KATIKA UKUMBI WA GOLD CREST JIJINI MWANZA.
SHUGHULI NZIMA INASIMAMIWA NA STOPPERS ENTERTAINMENT.
BURUDANI ITATOLEWA NA LINAH, DITTO NA HAFSA KAZINJA.
MSHEHERESHAJI MKUU AU MC WA SHUGHULI NZIMA NI MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOKA KUNDI LA ORIGINAL KOMEDI.

Amina.
Brenda.
Cecy.
MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS JAKAYA KIWETE JIJINI ARUSHA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Zanzibar katika Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha
PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana wa Arusha walioshiriki kutoa huduma kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wakati wa hafla ya chakula cha usiku baada ya ufunguzi wa mkutano huo Mei 31, 2012 usiku katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Makamu wa Rais wa European Investment Bank Bw Plutarchos Sakellaris baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 31, 2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jengo hili liko nyuma ya jumba la mikutano la AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisamiana na Rais wa Japan International Cooperation Agency (JICA) Profesa Akihito Tanaka na baadaye kufanya naye mazungumzo baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Mshauri wa Mfalme wa Tano wa Morocco Bw Omar Kabbaj baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha
MIZENGO PINDA AMWAKILIHA RAIS JAKAYA KIKWETE KIKAO CHA SADC
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa kwa gwaride baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Luanda, Angola May 31, 2012 kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC. Anaongozwa na Waziri wa Nishati na Maji wa Angola Joao Baptista Borges. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Nishati na Maji wa Angola, Joao Baptista Borges baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Luanda nchini Angola May 31, 2012 ambako atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC Juni 1, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe baada ya kuwasili Luanda Angola May 31, 20121 ambako atamwakilisha Rais Jakaya Kikwenye katika Kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika SADC Juni 1, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengio Pinda akisalimiana na Rais wa Angola Jose Edwardo dos Santos katika kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleoo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC kilichofanyika Juni 1, 2012 Mjini Luanda Angola . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
BREAKING NEWS: SIMBA KUMTEMA MACHAKU
Kwa hisani ya www.bongostaz.blogspot.com
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Salum Machaku pichani anaweza kutolewa kwa mkopo kwa nusu msimu, ili ajifundishe adabu- kwani hivi sasa mabega yamepanda mno juu.
Habari ambazo zimepatikana kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Machaku amekuwa akijisikia mno baada ya kufanya vizuri kidogo msimu huu akiwa na jezi ya Wekundu wa Msimbazi, kiasi kwamba amekuwa akidharau hadi viongozi.
Kiongozi mmoja wa juu wa Simba,alisema kwamba uongozi ulifanya jitihada kubwa za kumbadili kitabia Machaku, ikiwemo kumuweka chini ya mchezaji anayeogopwa na wachezaji wote, Haruna Moshi ‘Boban’, lakini ikashindikana.
“Sasa tunataka tumpe nafasi ya mwisho, tumpeleke kwa mkopo klabu nyingine akacheze mzunguko mmoja tu, akijirekebisha, tunamrudisha, ikishindikana ndio imetoka,”alisema kiongozi huyo.
Wakati huo huo, Machaku ni kati ya wachezaji ambao wamo kwenye orodha ya nyota wanaotakiwa na mahasimu wa jadi wa Simba, Yanga. Na katika siku za karibuni, Machaku amekuwa karibu mno na kipa wa Yanga, Shaaban Hassan Kado ambaye waliwahi kucheza naye pamoja Mtibwa Sugar na timu ya taifa
DIAMOND AMSHUKURU WEMA 'LIVE' KUMFUNDA KIINGEREZA
Diamond na Wema enzi za penzi la shatashata, ambalo sasa limebaki historia
Kwa hisani ya Bongostarz.blog
MWANAMUZIKI nyota Tanzania, Diamond amesema kwamba kufanya kwake vizuri katika mahojiano aliyofanyiwa Kiingereza kwenye jumba la Big Brother Jumapili nchini Afrika Kusini, kulitokana na mafunzo mazuri ya kuzungumza lugha hiyo, aliyopewa na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu.
Diamond ameyasema hayo leo mchana katika kipindi cha XXL cha Clouds Radio- baada ya kuulizwa siri ya kujiamini kwake kuzungumza vema Kiingereza bila kitete alipokuwa akihojiwa BBA.
"Namshukuru sana mama yangu mzazi aliyenisomesha, lakini pia namshukuru Wema Sepetu English Course, kwa kweli alinisaidia sana wakati nipo naye kunifundisha kuzungumza Kiingereza kwa kujiamini,"alisema Diamond.
Diamond anakuwa msanii wa pili kuzungumza hadharani kunufaika na lugha ya Kiingereza kutoka kwa Wema, baada ya marehemu Steven Kanumba naye kuwahi kusema hapo awali, alisaidiwa mno na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 kunyoosha lugha huyo.

Subscribe to:
Posts (Atom)