Wednesday, June 13, 2012

UN YAWAHAMASISHA WATANZANIA KUJITOKEZA KUJITOLEA DAMU.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Dkt. Alberic Kacou akiongoza wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa kujitolea damu ikiwa ni wiki ya Kampeni ya Kitaifa ya kujitolea damu. Kulia ni Afisa Mtaalam wa damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Bw. Deochris Kaimukilwa.
Alberic Kacou akizungumza na waandsihi wa habari baada ya kumaliza zoezi la kujitolea damu ambapo amezungumzia changamoto Umoja wa Mataifa unazokabiliana nazo katika kufanikisha zoezi la kuhamasisha watu kujitolea damu ambapo ametaja moja wapo kuwa ni ugumu uliopo katika kuwashawishi watu kujitolea kutokana na fikra watu walizonazo kuhusiana na kujitolea damu.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akifanyiwa vipimo vya awali kabla ya kuchangia damu. Kulia Mtaalamu kutoka mpango wa Taifa wa Damu Salama Bi. Edith Senga.
Edith Senga akitoa tathmini kwa waandishi wa habari kuhusiana na zoezi zima la utoaji damu linavyoendelea nchini.

Na.Mwandishi wetu

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Watanzania wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kujitolea damu ili kufanikisha azma ya serikali ya kuwa na damu ya kutosha katika benki ya akiba ya damu.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kituo cha kijitolea damu kilichopo katika zahanati ya UN iliyopo Kinondoni, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou amesema Umoja huo unashirikiana bega kwa bega na serikali katika kuhamasisha kampeni ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama.

Katika kufanikisha kampeni ya kitaifa ya Kujitolea Damu, Umoja wa Mataifa umeweka utaratibu wa kuwa na vituo katika sehemu mbali mbali ambapo wananchi watakuwa wakijitolea damu, ambapo kwa kuanzia leo kituo kipo katika klinik ya UN ambako kwa kuonyesha mfano Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou amejitolea damu.


Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Hoyce Temu akizungumza leo amesema kesho tarehe 14 June 2012 ambayo ndio kilele cha Siku ya Kujitolea Damu Duniani, shughuli hiyo itafanyika katika Ofisi za Shirika la Afya Duniani – WHO zilizopo mkabala na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.


Aidha amewataka wananchi jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha lengo la Siku ya Kujitolea Damu Duniani, na kuwatoa hofu kuwa sio kweli kwamba ukijitolea damu unapimwa virusi vya ukimwi au damu yako itapungua. Viongozi katika ngazi mbalimbali na watu wote mashuhuri wanatakiwa kutumia nafasi walizonazo kuhamasisha watu kuchangia damu.

PODOLSKI NA MULLER WALIFELI DHIDI YA URENO: JE REUS NA SCHURRLE WATAANZA DHIDI YA UHOLANZI.

Mchezo wao kwanza wa Euro 2012 ulienda kwa mujibu wa Ujerumani walivyotaka - kwa upande wa matokeo, lakini vijana wa Joachim Low hawakuonyesha uwezo mkubwa ambao wengi walikuwa wakiutegemea dhidi ya Ureno. Ushindi wa 1-0 ulikuwa ni bahati kwa timu hiyo kwa kuwa hata Ureno walipoteza sana nafasi kwa kutokuwa na bahati waliyoipata Ujerumani.

Ndio maana haishangazi kuona umma wa Ujerumani ukitegemea kuona mabadiliko kwenye mechi zijazo, kwa kuwa hawakuona timu yao ikicheza kwa kutengeneza nafasi nyingi za magoli dhidi ya kikosi cha Paulo Bento. Low alifanya uamzui mkubwa kwa kumchezesha Mats Hummels na Mario Gomez, lakini mashabiki wanataka kocha wao aongezee ujasiri wakati wa mechi zijazo.

Kuna maswali juu ya nafasi mbili: Thomas Muller na Lukas Podolski wote wanaweza wakaanzia benchi kwenye mechi zijazo. Wote walionyesha kwamba wapo tayari kucheza kwa kujituma bila kuchoka lakini kiukweli hawakucheza vizuri, na sasa Marco Reus na Andre Schurrle wanaweza kuwa wabadili wao dhidi Uholanzi?

Akiwa mmoja ya chipukizi bora wa ligi ya Ujerumani msimu uliopita, kiwango cha Marco Reus akiwa Borussia Monchengladbach kimeonyesha ubora anaoweza kuuleta ndani ya kikosi: akiwa na na rekodi nzuri za ufungaji na ubunifu mzuri kiwanjani. Kwa upande wa Schurrle amekuwa katika form nzuri kwa siku za hivi karibuni katika mechi za kirafiki kuelekea kwenye Euro, pia alikuwa na msimu mzuri na Bayern Leverkusen, na hakuna ubishi kwamba amaelata maswali mengi juu ya nani aanze kati yake na Podolski.

PAZIA LA EBSS KUFUNGULIWA RASMI DODOMA MWAKA HUU.


Na Mwandishi Wetu Dodoma
IKIWA kesho kutwa (Juni 16) ndio pazia la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS) linafunguliwa rasmi kwa kuanza kutafuta vipaji mkoani Dodoma ambapo maelfu ya  watu wameonesha nia ya kujitokeza kushiriki.

Mkoani hapa vijana wengi wameonesha kuwa na shauku kubwa ya kusubiria kushiriki katika usaili huo ambapo unaanza rasmi keshokutwa (Jumamosi ya Juni 16) katika ukumbi wa Royal Village.

Shauku hiyo inaweza kuwa inasababishwa na dau la zawadi la milioni 50 lililotangazwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel lakini pia dili la kuendelezwa kisanii ambalo nalo linawavutia vijana zaidi.

Akizungumzia usaili wa kesho kutwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampun ya Benchmark Production Ritha Paulsen alisema kuwa usaili wa mwaka huu watachukua washiriki kuanzia miaka 16 na kuendelea.

Alisema kuwa uamuzi huo wa kuchukua washiriki wa kuanzia miaka 16 ni kuwapa nafasi wale wenye uwezo wa kuimba na kupanga sauti ili nao wajaribu bahati yao.

“Najua kwa mwaka huu kwa kuwa shindano hili linadhaminiwa na Zantel hivyo mambo yamekuwa ni makubwa zaidi na napenda kuwaomba vijana kujitokeza kwa wingi zaidi kutumia fursa hii ambayo Zantel inawapatia mwaka huu” alisema Ritha.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Ali Bin Jarsh akizungumzia shindano hilo alisema kuwa Zantel inatambua nafasi ya muziki katika kukuza ajira na nchini.

Alisema kuwa Zantel imeamua kupitia Epiq Bongo Star Search kuinua vipaji vya vijana katika muziki ikiwa pamoja  na kuwatengenezea njia ya mafaniko.

KASEBA USO KWA USO NA CHEKA SIKU YA SABASABA.

Mabondia, Francis Cheka (kushoto) na Japhert Kaseba, wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao unaotarajia kufanyika Siku ya tarehe saba mwezi wa saba katika uwanja mpya wa taifa .Picha na Maktaba ya www.superdboxingcosach.blogspot.com)


Ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii nchini wakiongozwa na Diamond  pia kutakua na mechi ya Bongo Move na wasanii wa Bongo Fleva watakapochuana kwa mara nyingine katika mpambano uho ulioandaliwa na Global na kuratibiwa na Kaike Siraju utakuwa ni mpambano wa kwanza wa Masumbwi kufanyika katika uwanja mpya wa Taifa



Baadhi ya mabondia watakaosindikiza mpamnbano huo ni  Adiphoce Mchumia tumo atakaedundana na Ramadhani Kido wakati Amos Mwamakula ataoneshana kazi na Rashini Ali uku Mkongo Kanda Kabongo akizipiga na  Said Mbelwa wakati bondia chipkizi kutoka kambi ya masumbwi ya Ilala inayonolewa na Kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli Masta na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'Super D'  watampandisha bondia Ibrahimu Class kuoneshana kazi na Sadiki Momba

UNDER THE SAME SUN WALAANI KUENDELEA KWA MATUKIO YA MAUAJI YA ALBINO NCHINI

.

Afisa utetezi wa matukio ya mauaji  ya Albino kutoka Shirika la Under the Same Sun Bw, Kondo Seif akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi za Shirika hilo linalohusika na kutetea Maalbino nchini juu ya mauaji ya Albino yanayoendelea kutokea nchini Tanzania. Bw. Kondo alisema kuwa wanasikitika na kufadhaishwa na mauaji ya mwanaume asiyetambuliwa kati ya umri wa miaka 25-35 mwenye ulemavu wa ngozi yualiyofanyika  katika kijiji cha nambala kata ya Kikwe Tarafa ya Mbuguni  wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha . Alisema kuwa wamekuta mwili wake ukiwa umeharibiwa vibaya na kwamba ulikuwa umen'golewa sehemu kadha za viungo vya mwili wake vikiwemo mikono, masikio, ulimi,ngozi ya usoni,sehemu za makalio na sehemu zote za nyeti zake na nywele za kichwani. Alisema kuwa mwili wake umehifadhiwa katika hosipitali ya Mkoa Mount Meru. 
Afisa katika shirika la Under The Same Sun Bw, Gamanyo Mboya, akikazia unyanyasaji huo unaofanyika na watu wasiojulikana na alisema kuwa kuanzia january kufikia machi mwaka huu tayari wamepokea matukio sita ya kikatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambapo alisema kuwa kwasasa walemavu wa ngozi wamekuwa wakisafirishwa nje ya nchi na kwenda kuuawa alithibitisha hayo kwakusema kuwa walipata taarifa ya mtoto mwenye umri wa miaka 3 akisafirishwa kutoka Tanzania na kupelekwa  Bukinafaso.
3)
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini

TCAA YAKUTANA NA WADAU WA SEKTA YA ANGA JIJINI DAR LEO.

Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi  akifungua mkutano wa siku moja wa maboresho wa wadau wa sekta ya usalama wa Anga jijini  Dar es Salaam  Juni 13,2012,(kushoto) ni Mkurugenzi wa Sheria za Usalama wa mambo ya Anga kutoka Mamalaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)- Picha na Mwanakombo  Jumaa.
Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi (aliesimama) akifungua mkutano wa siku moja wa maboresho wa wadau wa sekta ya usalama wa Anga jijini  Dar es Salaam  Juni 13,2012,(kushoto) ni Mkurugenzi wa Sheria za Usalama wa mambo ya Anga kutoka Mamalaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)- Picha na Mwanakombo  Jumaa.
Baadhi ya wadau wa mkutano wa maboresho wa mambo ya usalama wa sekta ya usafiri wa Anga nchini wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano wa siku moja uliofanyika leo Juni 13,2012 jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) uliofunguliwa na Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Fadhili Manongi (hayupo pichani) Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali jinsi ya kuboresha usalama wa usafiri wa  anga pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa sekta hiyo. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Baadhi ya wadau wa mkutano wa maboresho wa mambo ya usalama wa sekta ya usafiri wa Anga nchini wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano wa siku moja uliofanyika  Juni 13,2012 jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) uliofunguliwa na Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Fadhili Manongi (hayupo pichani) Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali jinsi ya kuboresha usalama wa usafiri wa  anga pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa sekta hiyo. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mkaguzi  Mkuu anaeshughulikia masuala ya ajali za  usafiri wa ndege kutoka Wizara ya Uchukuzi  John Nyamwihura akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam( Juni13, 2012) kuhusu masuala mbalimbali ya usalama na ajali za ndege nchini katika mkutano huo wa siku moja wa wadau wa usafiri salama wa sekta ya anga

KASEBA,CHEKA, KUZICHAPA KWENYE TAMASHA LA USIKU WA TUMAINI.

 


Meneja Matukio wa Ukumbi wa Dar Live, Abdalah Mrisho, akitangaza tamasha hilo mbele ya wanahabari leo (hawapo pichani) katika ofisi za Global Publishers, zilizoko Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC), Ally Makaranga, akimkabidhi promota wa ngumi, Kaike Siraj (kushoto), hati kwa ajili ya mpambano kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba kwenye tamasha hilo.
Kaseba akijitapa kumchakaza Cheka kwenye pambano hilo.
Diamond akiahidi kutoa bonge la shoo tofauti na alizowahi kuzifanya.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Jacob Steven ‘JB’, akiahidi kuchezesha wasanii maarufu kwenye kikosi chake. Kulia ni Meneja Matukio wa Dar Live.
Mhariri wa gazeti la Championi, Phillip Nkini, (kushoto) akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Kaseba na mpambe wake wakiondoka eneo la tukio baada ya kumaliza mkutano.
Tamasha kubwa la burudani liitwalo ‘Usiku wa Tumaini’ linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7 mwaka huu. Katika tamasha hilo burudani mbalimbali zitakuwepo zikiwa ni pamoja na mechi ya soka kati wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Flava, mechi kati ya wabunge wapenzi wa Simba SC na wapenzi wa Yanga SC, muziki kutoka wanamuziki mbalimbali akiwemo mkali wa Bongo Flava, Naseeb Abdul ‘Diamond’, na pambano la ngumi kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba. Wasanii wataletwa uwanjani hapo kwa kutumia usafiri wa helkopta