![]() |
The 91 day reality super-series Big Brother StarGame, produced for M-Net’s AfricaMagic, is being screened live 24/7 on DStv 197 & 198. On Sunday 10 June South Africa’s Lee & Keagan and Namibia’s Junia & Jesica were randomly selected for nomination this week. For more information log on to www.africamagic.tv/bigbrother |
Monday, June 11, 2012
DJ FATTY WA XXL YA CLOUDS FM AKIKAMUA BIG BROTHER AFRICA JANA.
NMB YAIPA SERIKALI GAWIO LA BILIONI 7.9

Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa kwa niaba ya serikali amepokea sh 7.9 bilioni kutoka benki ya NMB ikiwa ni gawio la serikali kwa mwaka 2011 kama ilivoidhinishwa katika mkutano wake mkuu uliofanyika Juni 2, 2012.Gawio hilo lilitokana na serikali kumiliki asilimia 31.8 ya hisa katika benki ya NMB.
Akizungumza baada ya kupokea hundi hiyo jijini Dar es Salaam Dk. Mgimwa alisema, amefurahishwa na benki ya NMB kwa utendaji wake kwa kuwa mwaka 2010 iliweza kutoa sh bilioni 5.7 “Benki ya NMB inaonyesha dalili nzuri ya utendaji wake kwa kuwa ongezeko hili la mwaka 2011 la sh bilioni 7.9 kwa serikali ni ongezeko zuri na fedha hii iliyotolewa na NMB Imeweza kuichangia Serikali baada ya kupata faida kwa kuwa ni nyingi sana na itasaidia kuwalipa wafanyakazi wengi ” alisema Dk.Mgimwa”
Aidha, aliipongez NMB katika juhudi zake za kuisaidia serikali kupitia shughuli mbalimbali za kupambana na umasikini na kuboresha maisha ya wananchi wenye mahitaji. Alisema anathamini mchango wa NMB katika ukusanyaji wa kodi unaofanywa kupitia matawi yake yaliyosambaa Tanzania nzimai.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa NMB, Bw. Mark Wiessing alisema NMB itaendelea kuleta huduma nafuu za kifedha kwa jamii ya kitanzania katika maeneo yote ya vijijini na mijini “NMB imeweza kufikia wateja wake nchi nzima,pia imeweza kulipa kodi kwa serikali,ndio maana NMB ni benki bora kwa Tanzania
Tukio hilo muhimu lilishuhudiwa na manaibu wawili wa wizara ya Fedha na Uchumi, Katibu mkuu wa wizara ya fedha na manaibu wake watatu, mweka hazina mkuu, wakuu wa wizara zingine pamoja na wafanyakazi wa NMB
WAZIRI WA HABARI AZUNGUMZA NA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO WA SERIKALI LEO JIJINI MWANZA
![]() |
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Mwanza. |
Rais Kikwete awaapisha mabalozi Kumi Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete ashiriki kumuaga Muasisi wa CHADEMA Bob Makani katika viwanja vya Karimjee leo.
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mh. Freeman Mbowe wakati wa kuaga mwili wa Muasisi wa chama cha CHADEMA marehemu Bob Makani |
Rais Dkt.Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wakibeba jeneza la marehemu Bob Makani |
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za Mwisho |
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiteta jambo na mjumbe wa tume ya kukusanya maoni juu ya katiba Prof.Mwesiga Baregu katika viwanja vya Karimjee leo. |
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa katika viwanja vya Karimjee kufuatia msiba wa muasisi wa Chama hicho Bob Makani |
WANAFUNZI WA UDOM WAJITOLEA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula (Wa Pili Kushoto) akiwa amesimama wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe aliyeongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma, Na Balozi Job Lusinde katika zoezi la kujitolea damu kwa hiari lililofanyika siku ya leo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na Kuandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe akitoa neno fupi kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma waliofika katika Zoezi la Kujitolea Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma jana.
Afisa Mahusiano wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi Beatrice alipokua akitoa damu kwa hiari katika Zoezi la Kuchangia Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma jana huku Akishuhudiwa na Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Manongi(Mwenye Miwani)
Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika jana Chuo Hapo.
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akiaga wanafunzi na wafanyakazi waliojitoa katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) lililofanyika chuo hapo jana.Picha Zote Na Josephat Lukaza wa
Subscribe to:
Posts (Atom)