Saturday, June 16, 2012

MICHUANO YA KAGAME KUANZA JULAI 14.

 

Mashindano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) yanayoandaliwa na Baraza la Vyama ya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yatafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-29 mwaka huu ambapo timu zinatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya Juni 25 mwaka huu.
 
Yanga itashiriki mashindano hayo ikiwa bingwa mtetezi, wakati Tanzania Bara itawakilishwa na mabingwa wake Simba na Makamu bingwa Azam. Mashindano hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Chamazi pekee kwa sababu ya kupunguza gharama za uendeshaji.
 
Ratiba ya mashindano hayo yanayoshirikisha mabingwa kutoka nchi kumi na moja ambao ni wanachama wa CECAFA itapangwa Juni 29 mwaka huu.
 
Mashindano haya ni muhimu kwa CECAFA na Tanzania Bara ambayo ndiyo mwenyeji kwa maendeleo ya mpira wa miguu na pia kukuza kiwango cha mchezo huo kwa ukanda huu ambao kwa Afrika unaoongoza kwa kufanya mashindano mengi ya timu za Taifa pamoja na klabu.
 
Mwenyekiti wa CECAFA ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewaomba wadau kujitokeza kudhamini michuano hiyo ambayo itaoneshwa na kituo cha televisheni cha SuperSport. Pia amewataka washabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani kuunga mkono michuano hiyo.
 
CECAFA inawashukuru wadau wote kwa kuwezesha michuano hiyo kufanikiwa akiwemo Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa kutoa zawadi za fedha kwa washindi, Serikali ya Tanzania kwa kutoa Uwanja wa Taifa na Kamati ya Utendaji ya TFF kwa kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo

EDDA MISS KIGAMBONI CITY 2012.



Redds Miss Kigamboni City  2012 , Edda Sylvester (21) akipunga mono kwa furaha mara baada ya kutangazwa mshindi na kuvikwa taji la Kigamboni City katika shindano lililofanyika katika Ukumbi wa Navy Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Mroki Mroki) 

Warembo walioingia hatua ya tano bora ya Miss Kigamboni 2012, kutoka kulia Elizabeth Boniface, Ester Albert, Edna Sylvester, Hadija Kombo na Agnes Goodluck wakipozi kwa picha jukwaani baada ya kutajwa kuvuka nafasi hiyo na kupata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 baadea mwaka huu.

Warembo waliokuwa wakiwania taji la Miss Kigamboni City 2012 wakicheza show ya ufunguzi jukwaani.

Redds Miss Kigamboni City  2012 , Edda Sylvester (katikati) akiwa na mshindi wa pili Agnes Goodluck (kushoto) na mshindi wa tatu Elizabeth Boniphace mara baada ya kutangwazwa washindi. Edda aliwashinda warembo wengine 9 katika shindano hilo.