Thursday, June 7, 2012

"SITAKI UBABAISHAJI ATCL,ATAKAECHUKIZWA NA UAMUZI WANGU NA YEYE ATOKE-MWAKYEMBE"

Waziri wa uchukuzi Dr HARISON MWAKYEMBE,hii leo ameuelezea umma vigezo alivyotumia kumsimamisha kazi aliyekuwa Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege la Serikali ATCL Bw.Paul Chizi,kuwa ni utendaji mbovu ikiwa ni pamoja na Shirika hilo kuwapeleka maofisa wawili wa ATCL kusimamia zoezi la kushona sare 17 za wafanyakazi wa Shirika hilo Nchini China  kwa siku zaidi ya 45, ambapo walikuwa wakilipwa posho ya kukaa huko kila siku.Kigezo kingine ni kutokuwa na mipango thabiti ya kulifanya Shirika hilo kuwa la kujitegemea badala ya kubaki chini ya Serikali kila uchao. 
Mwakyembe ameonesha kushangazwa na baadhi ya waandishi wa habari nchini kukurupuka na kulitolea maoni suala hilo kinyume na hali halisi ilivyo

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015,CHADEMA HALALI MTU,OPERESHENI SANGARA YAPAMBA MOTO SASA WAMEFIKA MIKOA YA KUSINI MASASI MJINI,MAMIA YA WAKAZI WAJITOKEZA KUPIGANIA KADI.

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015,CHADEMA HALALI MTU,OPERESHENI SANGARA YAPAMBA MOTO SASA WAMEFIKA MIKOA YA KUSINI MASASI MJINI,MAMIA YA WAKAZI WAJITOKEZA KUPIGANIA KADI.







"SITAKI UBABAISHAJI ATCL,ATAKAE CHUKIZWA NA UAMUZI WANGU NAE ATOKE-MWAKYEMBE"

Waziri wa uchukuzi Dr HARISON MWAKYEMBE,hii leo ameuelezea umma vigezo alivyotumia kumsimamisha kazi aliyekuwa Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege la Serikali ATCL Bw.Paul Chizi,kuwa ni utendaji mbovu ikiwa ni pamoja na Shirika hilo kuwapeleka maofisa wawili wa ATCL kusimamia zoezi la kushona sare 17 za wafanyakazi wa Shirika hilo Nchini China  kwa siku zaidi ya 45, ambapo walikuwa wakilipwa posho ya kukaa huko kila siku.Kigezo kingine ni kutokuwa na mipango thabiti ya kulifanya Shirika hilo kuwa la kujitegemea badala ya kubaki chini ya Serikali kila uchao. 
Mwakyembe ameonesha kushangazwa na baadhi ya waandishi wa habari nchini kukurupuka na kulitolea maoni suala hilo kinyume na hali halisi ilivyo.

EURO 2012: ITALIA NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA WENDAWAZIMU, CASSANO + BALOTELLI KAZI IPO.


Maneno ya Cesare Prandelli alipomrithi Marcello Lippi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kombe la dunia mwaka 2010 ni kwamba ataifanya Azzuri ivutiwa kwa kucheza soka zuri la kushambulia. Kwa hakika amejitahidi sana huku akitambulisha utaratibu wa 'ethical code' (wachezaji wanaokuwa wamesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu hawatoitwa timu ya taifa) na kusisitiza katika kuwapa nafasi zaidi viungo wenye ufundi zaidi katika timu yake. Wazo ni kuifanya Italia kucheza kwa staili yake ya mfumo wa tiki-taka, staili inayopendelewa zaidi na Wahispania.

Akiuacha mfumo wa siku nyingi wa kujenga ukuta wa chuma na kucheza kwa mashambulizi ya kushtukiza kwa ajili ya mfumo ambao unatumia na Spain, ambao mpaka sasa umeleta matokeo ya mchanganyiko. italy haikufungwa hata mechi moja kwenye hatua ya kufuzu, lakini wamekuwa wakifungwa kwenye mechi za kirafiki. Skendo ya upangaji wa matokeo ambayo inaliandama soka la nchi hiyo kwa miaka mingi sasa, haitegemewi kuwa na madhara makubwa sasa hivi kuliko ilivyokuwa katika miaka 1982 na 2006, sababu kubwa ni kwa kuwa ni wachezaji wachache wa kikosi cha sasa wameguswa na kashfa hiyo, lakini suala hilo bado linabakia kuwa sio zuri kwa wachezaji.

Droo ya group C haikuwa nzuri kwa Italy, lakini atleast mechi yao dhidi ya Spain itakuwa ya kwanza. Na kupata pointi kutoka kwenye mechi hiyo ni jambo ambalo linawezekana, kwa kuangalia Spain huwa na kawaida ya kuanza vibaya michuano mikubwa, ukiangalia kombe la dunia lilopita walipofungwa na Uswis katika mechi ya kwanza makundi. Baada ya mechi hiyo atleast kidogo mambo yanaweza kuwa mazuri dhidi ya Croatia na Ireland.

WACHEZAJI MUHIMU

Gianluigi Buffon
Nahodha amerudi kwenye kiwango chake baada ya majeruhi yaliyomkumba msimu wa  2010-11. Ukifikiria namna safu ya ulinzi ilivyokuwa dhaifu, Azzuri wanahitaji kuwa na Buffon mwenye kiwango cha juu ili kuepeuka balaa. Ni uchizi sasa kufikiri kwamba safu ya ulinzi ambayo siku zote imekuwa ndio nguzo ya timu ya taifa ya Italia, sasa hivi ndio ulipo udhaifu wao, lakini hapa ndipo tulipo, na sasa tumaini lote lipo kwa Buffon na mikono pamoja na miguu yake kutatua hilo tatizo.


Mario Balotelli
Mario Balotelli alisema hatoshangilia goli mpaka atakapofunga goli la ushindi kwenye world cup au Euro, hivyo hii ndio nafasi pekee kumuona Super Mario akicheza kwa furaha baada ya kutupia kambani. Tuache utani, huu ni muda wake kuweza kuonyesha kwanini makocha wamuamini na kumpa nafasi. Balotelli ana nguvu, ujuzi na kimo kizuri, Anachohitaji ni kutulia na kutumia vizuri nafasi atakazopata huku akijiepusha na suala la nidhamu mbovu. Akifanikiwa kwenye hayo atatisha.


Daniele De Rossi
Katika kiungo ambacho kimejaa wapiga pasi mafundi zaidi, De Rossi ndio kiumbe anayetegemewa kusambaza minguvu yake. Shujaa huyu wa Roma ndio sasa anaelekea kwenye kilele chake, akiwa ameshaji-commit kwenye klabu yake, sasa yupo huru kufikiria timu ya taifa tu. Atakuwa na shughuli ngumu katika kupambana na kuizuia safu ya ulizni wa timu ambayo ni dhaifu kutoguswa

 JE SAFU YA USHAMBULIAJI YA MACHIZI ITAFANYA VIZURI?
Mara tu Giueseppe Rossi alipoumia, mikono ya Prandelli ilikuwa imefungwa. Akawa hana chaguo lingine zaidi ya kuwatumia Balotelli na Antonio Cassano. Hii haihusu suala la uwezo  - -wachezaji wote wawili wana vipaji vikubwa tataizo ni nidhamu: wote wawili wana matukio mengi ambayo yanahusu ukosefu wa nidhamu na tabia nyingine tofauti,ndani na nje ya uwanja. Hivyo hilo ni tatizo ambalo Prandelli inabidi alitafutie suluhisho

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015,CHADEMA HALALI MTU,OPERESHENI SANGARA YAPAMBA MOTO SASA WAMEFIKA MIKOA YA KUSINI MASASI MJINI,MAMIA YA WAKAZI WAJITOKEZA KUPIGANIA KADI.







RAIS KIKWETE NA MAKAMU WAKE DR BILAL WAMEAGANA NA BALOZI WA CANADA ALIYEMALIZA MUDA WAKE KWA NYAKATI TOFAUTI.



Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini Bwana ROBERT J. ORR ambae amemaliza muda wake wa uwakilishi, katika Ikulu ya Mjini Dar es Salaam.



Makamu wa Rais Dkt MOHAMMED GHARIB BILALakizungumza na Balozi wa Canada ROBERT J. ORR, aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.

UFREEMASON SIO SIRI TENA TANZANIA,WAWILI WAJIANIKA LEO TENA CLOUDS FM

 

Wadai wao wanafundisha dini zote na kudai kua kila mtu duniani ni Free masons na pia wafafanua maana halisi ya ufreemasons ila mwisho wasiku walishindwa kujibu kama wao ni mafreemasons au laaah! …



UFREEMASON SIO SIRI TENA TANZANIA.WAWILI WAJIANIKA LIVE CLOUDS FM KWENYE KIPINDI CHA LEO TENA.

akisikiliza maswali kwa ajili ya kujibu,anaye jiita freemason
      • akisikiliza maswali kwa makini — at clouds mikocheni.

  •  

  •  mmoja kati ya wanaojiita mafreemason
  • ''MKATABA WA YONDANI YANGA FAKE''RAGE


     

    Simba Sports club imesikitishwa na kitendo cha Young Africans kuvunja taratibu za usajili kwa kumrubuni mchezaji wake Kelvin Patric Yondani  kwa kuzungumza naye na baadae kwa ushahidi wa picha kuonekana wakimuandikisha makaratasi ambayo baadae imeripotiwa na vyombo vya Habari kwamba alikuwa akisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ya Young Africans. 
    Kwamba katika picha hiyo ameonekana mjumbe wa Young aliyejiuzuru bwana Seif Ahmed na hilo lilitoa shaka kama utaratibu huo umefanywa na klabu ya Young, lakini shaka hiyo imeondolewa pale ambapo tovuti ya Young imetangaza kumsajili mchezaji huyo wa Simba SC, lakini zaidi ya hilo picha inaonyesha fedha zikiwa zimewekwa mbele ya mchezaji jambo linaloonyesha mazingira ya kurubuniwa kwani kwa utaratibu wa kifedha, pesa nyingi kiasi hicho malipo yake yanashauriwa/yanapashwa kupitia benki. 
    Mbali ya hayo picha hiyo inamuonyesha Kelvin akiwa katika jezi ya mazoezi ya timu ya Taifa na yenye logo ya Kilimanjaro na kumbukumbu zinaonyesha mkataba kati ya TBL na TFF tarehe 9/5/2012, kwa haraka haraka tukio hilo limefanyika katika kipindi chini ya mwezi mmoja ingawa taarifa za ushahidi zinaonyesha tukio hilo limetokea jana tarehe 6/6/2012.
    Simba Sports Club ilipenda kuamini kwamba tukio hilo haliihusu klabu ya Young kwani bwana Seif Ahmed alishajiuzuru kutoka kwenye kamati ya Young Africans, kwani Young ni klabu kongwe na inayojua taratibu zote za usajili.
    Kwamba Simba Sports Club imeshawasiliana na jopo lake la mawakili na inajiandaa kuishtaki klabu ya Young katika chombo husika cha mpira na kudai adhabu ya kutopitisha majina yote ya usajili ya Young kwa mwaka 2012/2013 na miaka mingine miwili ijayo na Simba SC ipo tiyari kufuatilia suala hili hadi katika mahakama ya mpira ya FIFA.
    Kelvin Yondani ni mchezaji halali wa Simba Sc aliye na mkataba hadi 31 mei 2014 mkataba ulioongezwa tarehe 23/12/2011 kuundeleza mkataba wa awali uliokuwa unaisha tarehe 31/5/2012. Sheria za FIFA za hadhi na uhamisho wa wachezaji ziko wazi  katika kipengele cha 5 kifungu kidogo cha 2 kinasema kwamba mchezaji atasajiliwa kuichezea timu moja tu kwa wakati mmoja.

    JE ROY HODGSON NI CHAGUO SAHIHI KWA ENGLAND?

                    
    kama ilivyokuwa ada kwa mashabiki wengi wa english premier league naona ya kwamba roy hodgson siyo chaguo sahihi la kuwa coach wa england kwa sababu kitendo cha kumuacha Rio Ferdinand kilikuwa si cha uana michezo  kwa sababu baada ya kuumia gary cahil mashabiki wengi wa soka walijua mtu ambaye atakuja kuchukua nafasi  yake ni Rio Ferdinand lakini badala yake amemuita Martin Kerry beki ambaye amecheza mechi moja ya kimataifa na mechi yenyewe ilikua zidi ya norway na aliingia dakika mbli za mwisho huku Rio ferdinand akiwa  amecheza mechi 81 za kimataifa na pia msimu huu akicheza mechi 36 za manchester united na kumaliza na kusema Rio Ferdinand kuachwa  katika timu ya taifa sio swala la uanamichezo bali ni mgogoro uliokuwepo kati yake na John Terry hii n kutokana John Terry kumbagua mdogo wake Anton Ferdinand                                              

    ukiachana na kutoitwa kwa Rio Ferdinand pia uamuzi wa Roy Hodgson kumuita Stewart Downing zidi ya Adam Johnson pia ni uchaguzi usio sahihi kwa sababu tumuangilie mtu kama Stewart Downing msimu huu amaeheza mechi 36 za league na Hana goli hata moja ukiacha na kutofunga pia hana hata assits hata moja je mtu huyo kwenye mashindano ya mwezi mmoja atakupa mchango gani?