Saturday, June 2, 2012

JESHI LA POLISI ZANZIBAR LASITISHA MHADHARA WA UAMSHO

 
JESHI la Polisi Zanzibar limepiga marufuku maandamano na mihadhara ya aina yoyote visiwani hapa hadi hapo itakapotangazwa tena.
Taarifa ya Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imesema kuwa hatua hiyo inatokana na agizo la Serikali la kusitisha shughuli zote za mikusanyiko ya vikundi vya kidini vikiwemo vile vyenye usajili na ambavyo havina ili kuepusha uvunjifu wa amani.
Akisisitiza msimamo huo wa Jeshi la Polisi, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kwa mtu ama kikundi chochote kitakachokaidi agizo hilo kwa lengo la kudumisha amani na usalamawa viisiwa hivyo.
Kamishna Mussa amesema Jeshi la Polisi limelazimika kutoa msisitizo huo kufuatia taarifa za viongozi wa kikundi cha Uamsho kuwatangazia wananchi kuwa kesho wangefanya mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba kinyume na maagizo ya Serikali.
Amewataka Wananchi wakiwemo waumini wa dini zote kutojitokeza kushiriki mhadhara huo na mihadhara mingine itakayotangazwa katika kipindi hiki cha marufuku ya mikusanyiko ya aina hiyo.
Jana akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar, Kiongozi wa Kikundi cha Uamsho Sheikhe Farid Hadi, alisema wangefanya mhadhara mkubwa hiyo kesho jioni na kufanya maandamano Jumanne ya Juni 26, mwaka huu

UJUMBE WA MAREKANI WAONANA NA RAIS DK.SHEIN

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Seneta wa Marekani Christopher
Coons,akiwa na Ujumbe aliofuatana nao  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar
leo,kuzungumza na Rais.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Seneta wa Marekani Christopher
Coons,akiwa na Ujumbe aliofuatana nao  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar

MISS SINGIDA YAFIKIA KILELE

 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akikabidhi zawadi Zena Mode, baada kuibuka mshindi, shindano la Miss Singida, lililofanyika usiku wa kuamkia leo, Juni 2, 2012 katika ukumbi wa Aqua mjini Singida. Mshindi wa kwanza amepata sh. 400,000, wapili sh. 300,000 na wa tatu sh. 200,000.  Akifungua shindano hilo, Nape ameahidi kwamba CCM itatoa ajira kwa miss Singida kama atafanikiwa kuingia katika tatu bora katika shindano la Miss Tanzania.na kwamba CCM inayatambua mshindano ya urembo hapa nchini.

Nape akiwa na Miss Sgd, Zena Mode. wengine ni mshindi wa pili Rehema Marwa na  mshindi wa tatu, Eliza Diamond

. Warembo walioingia tano bora
Msanii Khadija Kopa akitumbuiza mashabiki wakati wa shindano hilo mjini Singida

Rais Kikwete akutana na Mmiliki wa klabu ya Portsmouth Dkt. Sulaiman Al Fahim Ikulu jijini Dar es Salaam leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim wakati walipokutana leo, Jumamosi, Juni 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam. Dkt. Al Fahim ambaye ni mwenyekiti wa zamani na mmiliki mwenza wa Klabu ya soka ya Portsmouth ya Uingereza yuko nchini kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika uchumi wa Tanzania. Dkt. Al Fahim pia ndiye aliyeongoza mazungumzo na kununuliwa kwa klabu bingwa ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Manchester City na Kampuni ya Arabuni. (Picha na fredy Maro).
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mzungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim mara baada ya  mazungumzo yao Ikulu leo.

BREAKING NEWS: FLOYD MAYWEATHER AANZA KIFUNGO CHA MIEZI 3 - 50 CENT AMSINDIKIZA JELA

 
Bondia Floyd Mayweather leo ameanza kifungo cha miezi 3 jela alichohukumiwa mwezi Desemba mwaka jana kutokana na kuvunja sheria kwa kufanya ugomvi. Wakati akielekea Jela Mayweather alisindikizwa na rafiki yake kipenzi mwanamuziki 50 Cent.
Mayweather akitiwa pingu na polisi kuelekea kwenye karandinga.
"Nenda dogo nitakumiss kaka yako" 50 Cent na Mayweather.
Hiki ndio chumba atakachokaa Mayweather kwa miezi 3
Hizi ndio sare zake kwa kipindi chote atakachokaa jela.

KUTOKA KWA PLATINI MPAKA DAVID VILLA: WATU SABA WALIOITAWALA MICHUANO YA EURO


Mastaa wengi wamewahi kung'ara kwenye michuano ya Ulaya - lakini ni wachache wameweza kutawala kama majembe haya.

Huku michuano ya nchini Poland na Ukraine ikiwa karibuni kuanza, tunachukua nafasi hii kukuletea watu saba ambao waliwasha moto wa kutisha kwenye historia ya michuano ya Euro

MICHEL PLATINI

MARCO VAN BASTEN

PETER SCHMEICHEL

ALAN SHEARER

ZINEDINE ZIDANE ZIZZU

DAVID VILLA

KUTOKA KWA PLATINI MPAKA DAVID VILLA: WATU SABA WALIOITAWALA MICHUANO YA EURO

 

Mastaa wengi wamewahi kung'ara kwenye michuano ya Ulaya - lakini ni wachache wameweza kutawala kama majembe haya.

Huku michuano ya nchini Poland na Ukraine ikiwa karibuni kuanza, tunachukua nafasi hii kukuletea watu saba ambao waliwasha moto wa kutisha kwenye historia ya michuano ya Euro

EXCLUSIVE INTERVIEW NA KOCHA WA UJERUMANI: TIMU YANGU INA NJAA NA MACHO YOTE TUMEWEKA KWENYE LENGO LA KUTWAA EURO 2012

Katika kuelekea michuano ya EURO 2012, nilitafuta nafasi ya kuonana na kocha wa timu wa timu ya taifa ya Ujerumani nikiwa nchini humo nilipoenda kwa madhumuni ya kuangalia fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya. Nilifanikiwa kuonana na Joachim pamoja na mchezaji Mario Gomez na kufanya mahojiano kuhusu michuano ya Euro 2012 na nafasi ya Ujerumani kwenye Michuano hii.
Kwa kuanzia tuanze na interview na kocha Low na ilikuwa kama ifuatavyo.


Shaffih: Unajisikiaje kupangwa kwenye group ambalo wengi wanaliita kundi la kifo?

Low: Kwa sura ya kundi, tumepangwa kwenye kundi ngumu zaidi kuliko yote. Uholanzi na Portugal  zote ni timu zenye wachezaji wa daraja la dunia na mechi zao dhidi yetu zitakuwa ni ngumu sana; nadiriki kusema mechi kufa na kupona. Kwa upande wa Denmark, kwa miaka kadhaa wameshaonyesha kwamba wanaweza kushindana kwenye michuano mikubwa. Hawaogopi timu zenye majina makubwa na hawana cha kupoteza na hilo linawafanya wawe hatari zaidi na wasiotabirika. Kwa maana hiyo nasema kwamba kila timu kwenye kundi B ina nafasi ya kupita.



Shaffih: Mliwamaliza na kuwazidi kwa kila kitu Uholanzi kwenye mechi ushindi wa 3-0 mwezi November. Hilo linakupa nguvu yoyote kisaikolojia?

Low: Usiku ule tulicheza soka la aina yake na la kipekee na ndio maana tukapata matokeo chanya kutoka mchezo ule. Uholanzi tutakayokutana nayo kwenye Euro itakuwa na nguvu zaidi na yenye kubadilika sana hilo nina uhakika.



Shaffih: Je rekodi yenu nzuri kwenye hatua ya kufuzu inaweza kuwaletea matatizo yoyote kwa maana ya wachezaji kujiamini sana?
Low: Sina wasiwasi kabisa kwenye matokeo yale. Kikosi nilichonacho kina njaa ya mafanikio, na kipo focused  kwenye lengo la kushinda kikombe. Hakuna aliye kwenye fikra kama tulimaliza kazi kwenye kufuzu tu japokuwa tulifanya vizuri sana.


Shaffih: Ujerumani wanaangaliwa kama moja ya timu zinazopewa nafasi sana na imani ipo juu hapa Ujerumani kwamba mnaweza kubeba kombe . . .
Low: Baada ya kufanya vizuri kwenye kufuzu, mategemeo yamepitiliza. Lakini droo ya kundi tulilopangwa kidogo imeshusha mategemeo. Sasa watu wanaangalia hali halisi kidogo. Lolote linaweza kutokea kwenye michuano. Majeruhi yanaweza yakabadilisha kila kitu. Kama makocha wengine, nitakuwa naomba tuepukane na balaa hilo na tumalize michuano tukiwa tuo salama ili kuweza kukamilisha ndoto ya ubingwa wa Euro 2012.


Shaffih: Nini nguvu yenu?
Low: Moja ya vitu vikubwa kwangu mimi ni kuona namna tulivyojimaarisha na kuendelea kuja kuwa timu ya ukweli, ambayo ina umoja ambao ndio nguzo yetu. Hakuna mchezaji ambaye moja kwa moja anajiangalia yeye. Kila mmoja wetu anamsaidia mwenzake, tunashirikiana kuiletea mafanikio timu yetu, na pale vijana wapya wanapokuja wanakuta mfumo huo na kuumudu vizuri. Spirit ya timu ilikuwa juu sana kwenye WOZA 2010 PALE South Africa  na hili limeendelea mpaka leo.


Shaffih: Je Euro 2012 inaweza ikawa vita ya kwenu pamoja na Spain?
Low: Spain wapo vizuri sana lakini sio kama ndio wagombea taji pekee. Uholanzi na timu nzuri sana. Siku zote nimekuwa na heshima kubwa juu ya uwezo wa Ureno, France wanaimarika, na tusiwatoe England..

KIKOSI CHA ENGLAND EURO: RIO FERDINAND ATOSWA: CARROLL NA CHAMBERLAIN NDANI

Wednesday, May 16, 2012

KIKOSI CHA ENGLAND EURO: RIO FERDINAND ATOSWA: CARROLL NA CHAMBERLAIN NDANI

Joe Hart gives instructions during the International Friendly match between England and the Netherlands at Wembley
Joe Hart (Manchester City)

England squad:

Goalkeepers: Joe Hart (Man City), Rob Green (West Ham), John Ruddy (Norwich)

Defenders: Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Man Utd), John Terry (Chelsea), Joleon Lescott (Man City), Gary Cahill (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Leighton Baines (Everton)

Midfielders: Theo Walcott (Arsenal), Stewart Downing (Liverpool), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Steven Gerrard (Liverpool), Gareth Barry (Man City), Frank Lampard (Chelsea), Scott Parker (Tottenham), Ashley Young (Man Utd), James Milner (Man City)

Forwards: Jermain Defoe (Tottenham), Wayne Rooney (Man Utd), Danny Welbeck (Man Utd), Andy Carroll (Liverpool)

Robert Green in action for England
Robert Green (West Ham)

Getty

John Ruddy
John Ruddy ()Norwich)

Getty

Glen Johnson prepares to take a throw in during the international friendly match between England and Spain at Wembley
Glen Johnson (Liverpool)

Getty

Ashley Cole in action for England
Ashley Cole (Chelsea)

Getty

Phil Jones in action for England
Phil Jones (Manchester United)

Getty

Gary Cahill in action for England
Gary Cahill (Chelsea)

Getty

John Terry in action for England
John Terry (Chelsea)

Getty

Joleon Lescott of England in action
Joleon Lescott (Manchester City)

Getty

Leighton Baines in action for England
Leighton Baines (Everton)

Getty

Frank Lampard
Frank Lampard (Chelsea)

Mirror

Gareth Barry in action for England
Gareth Barry (Manchester City)

Action

Steve Gerrard in action for England
Steven Gerrard (Liverpool)

Getty

Scott Parker in action for England
Scott Parker (Tottenham)

Getty

James Milner in action for England
James Milner (Manchester City)

Getty

Ashley Young in action for England
Ashley Young (Manchester United)

Getty

Theo Walcott in action for England
Theo Walcott (Arsenal)

Getty

Stewart Downing of England
Stewart Downing (Liverpool)
Alex Oxlade-Chamberlain in action for the Under 21s
Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal)

Getty

Jermain Defoe in action for England
Jermain Defoe (Tottenham)

Getty

Andy Carroll in action for England
Andy Carroll (Liverpool)

Getty

Wayne Rooney in action for England
Wayne Rooney (Manchester United)

Getty

Danny Welbeck in action for England
Daniel Welbeck (England