Saturday, June 23, 2012

OKWI AGEUKA LULU SOKO LA USAJILI: BAADA YA ORLANDO, SASA TIMU YA SERIE A NA MAMELOD SUNDOWNS ZAGOMBEA SAINI YAKE

 

Nyota ya jaa ya mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na Uganda Emmanuel Okwi, inazidi kuwaka, siku chache baada ya klabu bingwa ya Orlando Pirates kutuma barua ya kutaka mshambuliaji huyo wa Simba aende kufanya majaribio kwenye klabu hiyo, leo hii timu pinzani ya Orlando kwenye ligi ya Afrika kusini, Mamelodi Sundowns wameuambia uongozi wa Simba kwamba wapo tayari kumnunua mshambuliaji huyo.

Taarifa zilizothibitishwa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kwamba Mamelodi wametuma maombi ya kutaka kumsaini Okwi ambaye amekuwa na msimu mzuri sana ndani na nje ya ligi kuu ya Vodacom msimu ulioisha.

Pia chanzo changu hicho cha habari kutoka ndani ya Simba kilisema kwamba kuna timu moja inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A, wameonyesha nia ya kumtaka Okwi lakini wamesema kwamba wanasubiri mpaka michuano ya Euro itakapoisha ndipo watakapoamua juu ya suala la usajili wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda.

CHEMSHA BONGO: UNAWAJUA WACHEZA SOKA WEWE? WATAJE HAWA WOTE KWA MAJINA.

 


Hiki ni kikosi cha moja ya timu zilizoshiriki kwenye Euro 2012.
After a year of scandals, this Barking-born boy is aiming to be crowned champion of Europe for the second time in just two months
2
He shed the unfortunate fringe and has gone on to become England's midfield enforcer and Mr Reliable
1

 
All all-round athlete who excelled at cricket and athletics, this England regular recently won his first league title
5
He replaced Rio Ferdinand, and then Gary Cahill in the England back four, but has been one of the stand out stars of Euro2012 so far
4:


England's youngest ever player, this Londoner has shone so far this summer as manager Roy Hodgson's super sub
8
6: He was tall, even as a schoolboy, but didn't take up football until he was 15 - preferring cricket during his early years.
7


8: England's new captain fantastic, a deadball specialist who has shone with the armband this summer
9   
9: The baby of the team, this photo is barely a decade old. This star in the making is a second generation England player 
14: There's no mistaking that mischievous grin. Back after a break, England fans are praying we've not seen the best of him yet
12: The baby face is long gone on this star, arguably England's best player and the best in the world in his position. If England make the final, it'll win him his 100th cap13: A child footballing prodigy who's living up to his hype. Scorer of one of the best goals of the tournament so far11: England's first choice number 2 and a solid performer in Poland/Ukraine. One of 6 Liverpool players hoping to find success this summer
10: A regular in the England set-up, he shrugged off a personal tragedy to compete at Euro2012, where he hopes to win his 50th cap
Add caption
                                         10

7: Went to the same school as Gazza and followed in his footsteps to Newcastle and then England
10

WANAFUNZI WA MUHIMBILI WACHANGIA DAMU KATIKA MPANGO WA DAMU SALAMA

Mtaalamu wa Maabara kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Eliza Mgaya, akiweka vizuri mfuko wa damu kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo Cha Afya Muhimbili Paul Boniface, ambaye ameshiriki kwenye zoezi la kujitolea damu linaloenda sambamba na upimaji wa bure wa magonjwa mbalimbali, linaloratibiwa na Wanafunzi wanao hitimu mafunzo ya Maabara kwenye Chuo cha Maabara Muhimbili
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakijiorodhesha Hospitali ya taifa Muhimbili ili kuweza kupata huduma za bure za kupima afya zao, zoezi hilo linaratibiwa na wanafunzi wa maabara wanao maliza kwenye chuo cha maabara cha Muhimbili.
Wanafunzi wanaohitimu ngazi za Astashada na Stashahada za Maabara kwenye Chuo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambao ndio walioandaa zoezi la upimaji afya linaloendelea hapa Muhimbili wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye hafla yao ya kuhitimu masomo ambapo wanaelekea kuhitimisha masomo hayo

Hilda Edward ndiye Miss Dar Inter College 2012

 

Miss Dar Inter College 2012, Hilda Edward akipongezwa baada ya kushinda kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho, katikati ya Jiji la Dar es Salaam usiku huu.
Hapa Hilda akipigana busu moto moto la pongezi na Miss Dar Inter College aliyevua taji Blessing Ngowi. Picha kwa hisani ya http://bongostaz.blogspot.com/
Hii ndiyo tano bora  Kutoka kulia Veronica Yole, Sada Suleiman, Rose Muchunguzi, Jamila Hassan na Hilda Edward
DIAMOND PLATINUM;  Nassib Abdul akitumbuiza kwa hisia, kibao Wema Wangu mbele ya jaji Wema Sepetu, ilikuwa tamuuu
INAUMA UCHUNGU; Katikati Jaji Wema akifuatilia kwa hisia zote kibao Wema Wangu wakati Diamond the Platinum anatumbuiza...

MISS EAST AFRICA 2012 (MALAWI)



 Miss Elidas Ella Chirwa (22)
Miss Elidas Ella Chirwa (22)

Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Malawi katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ametangazwa rasmi baada ya kuwashinda wenzake 39 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Malawi katika mashindano hayo.

Mrembo huyo ni Miss Elidas Ella Chirwa (22) mwenye urefu wa 1.82m ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo kikuu cha Malawi

Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam