Saturday, June 23, 2012

WANAFUNZI WA MUHIMBILI WACHANGIA DAMU KATIKA MPANGO WA DAMU SALAMA

Mtaalamu wa Maabara kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Eliza Mgaya, akiweka vizuri mfuko wa damu kutoka kwa mwanafunzi wa Chuo Cha Afya Muhimbili Paul Boniface, ambaye ameshiriki kwenye zoezi la kujitolea damu linaloenda sambamba na upimaji wa bure wa magonjwa mbalimbali, linaloratibiwa na Wanafunzi wanao hitimu mafunzo ya Maabara kwenye Chuo cha Maabara Muhimbili
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakijiorodhesha Hospitali ya taifa Muhimbili ili kuweza kupata huduma za bure za kupima afya zao, zoezi hilo linaratibiwa na wanafunzi wa maabara wanao maliza kwenye chuo cha maabara cha Muhimbili.
Wanafunzi wanaohitimu ngazi za Astashada na Stashahada za Maabara kwenye Chuo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambao ndio walioandaa zoezi la upimaji afya linaloendelea hapa Muhimbili wakifuatilia hotuba mbalimbali kwenye hafla yao ya kuhitimu masomo ambapo wanaelekea kuhitimisha masomo hayo

No comments:

Post a Comment