Sunday, May 27, 2012

Meneja Twanga Pepeta atimuliwa kazi


Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka amesema kuwa wamemfukuza kazi Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Asha alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa Sospeter anaihujumu bendi kwa kuwashawishi wasanii kuihama bendi hiyo ili watue bendi ya Mashujaa ambayo naye ana mipango ya kutua huko.

"Tumeamua kumfukuza kazi Meneja wa Twanga Pepeta, Sospeter kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ubadhirifu na kutowajibika ipasavyo... anasuka mipango ya kwenda bendi ya Mashujaa, hivyo tumeamua kumuondoa mapema ili aende akiwa huru.

"Tumemwandikia barua ya kumfukuza kazi na pia anapaswa kulipa fedha za matamasha alizokwapua... nimeamini kumbe kikulacho kinguoni mwako," alisema Asha.

Pia alisema sababu nyingine ya kumtimua ni kukosa uaminifu baada ya kupokea fedha za matamasha mbalimbali takriban sh. milioni 6, lakini hajaziwasilisha ofisini kama ilivyo utaratibu wa kazi.

Asha alisema uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu kumhusu Sospeter umebainika kuwa ndiye amekuwa mstari wa mbele kuwashawishi baadhi ya wasanii wa Twanga Pepeta waliohamia Mashujaa na yeye ana mpango wa kuhamia katika bendi hiyo, hivyo anawatanguliza wasanii ili iwe rahisi yeye kujiunga nao atakapokamilisha dhamira yake.

"Mashujaa wenyewe wanadai eti Sospeter anajua siri nyingi za mafanikio ya Twanga Pepeta, hivyo atawasaidia kuimarisha bendi yao, tumeamua kumfukuza ili akawape vyema hizo siri," alisema Asha.

Mkurugenzi huyo alisema imebidi wamfukuze akajiunge na bendi hiyo anayoona anataka kuitumikia na kwamba safari aliyokwenda  Nyanda za Juu na bendi hiyo ndiyo ya mwisho katika utumishi wake akiwa na Twanga Pepeta.

Mbali ya hujuma za fedha na wasanii walioikimbia Twanga Pepeta kuhamia Mashujaa, Asha alisema kuwa imegundulika kuwa, Sospeter hivi sasa anamshawishi mpiga gita la besi wa bendi hiyo, Jumanne Said 'Jojo Jumanne' ili ahamie Mashujaa, hali aliyosema kuwa haiwezi kuvumiliwa kuendelea kuitafuna bendi hiyo.

"Tumemchunguza na kujiridhisha kumhusu huyu meneja Sospeter, ni mtu asiyeitakia uhai Twanga Pepeta... kama hilo ndilo lengo lake akafanye kazi na hao wanaomhitaji na mimi niendelee na mipango yangu na watu ninaoamini kuwa watanisaidia kuikuza tasnia ya muziki wa Twanga Pepeta," alisema Asha.

DIAMOND PLATINUM AINGIA SOUTH AFRICA KWAAJILI YA KAZI MOJA TU>>>>>KUTOA BURUDANI

DIAMOND PLATINUM AINGIA SOUTH AFRICA KWAAJILI YA KAZI MOJA TU>>>>>KUTOA BURUDANI

Mtu mzima Diamond amedondoka pande za South Africa tayari kwa burudani kali kabisa kwa watanzania waishio pande za Durban na Capetown. Nilivyowasiliana nae dakika 10 zilizopita asubuhi hii ameniambia usiku wa kuamkia leo jumapili alikuwa na show Capetown so baada ya hapo nadhani itakuwa Joburg 

Huyu ndio promota aliyemleta Diamond South Africa kupiga show 

Diamond akiwa na Wasafi wa SA

TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI MAGUNIA 50 NA WATUHUMIWA WANNE MKOANI ARUSHA

TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI MAGUNIA 50 NA WATUHUMIWA WANNE MKOANI ARUSHA

Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akiwaonyesha waandishi wa habari shehena ya mifuko 50 ya bangi iliyokuwa kwenye gari baada ya kukamatwa tarehe 23/05/2012 wilayani Longido (PICHA NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA)
Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akihoji jambo kwa watuhumiwa hao.
Mchezaji wa Judo kutoka CCP Polisi Moshi (wa juu) Bw. Kisamerwa Magangwa akiwa amemgeuza mshindani wake Bw,.Mohammed Juma kutoka Magereza  Ukonga jijini Dar es Salaam katika mchezo huo.
Baadhi ya mashabiki walioudhuria katika
mpambano wa mchezo huo wakifuatilia kwa makini.
Wataalamu wa kufuatilia muda katika mashindano ya mchezo huo wakifuatilia kwa umakini mchezo huo.

Mashindano ya Mchezo wa Judo yaanza rasmi

Rais wa Judo Tanzania Bw, Khalifa Kiumbemoto katikati akifuatila kwa makini Mashindano ya Mchezo huo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Landmark  jijini Dar es Salaam wa kwanza kushoto kwake ni Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Habari na Michezo Bw. Charles Mattoke  na wapili kushoto kwake ni Mdhamini wa Mashindano hayo kutoka Germin Copperation LTD Bw. Yulliy Tarverdyan. Katika Mashindano hayo Watanzania walionekana kushindwa na wachezaji kutoka Zanzibar.

Hali yaanza kuwa shwali Visiwani Zanzibar

Polisi wakutuliza ghasia wakitawanya waandamanaji visiwani zanzibar

Kanisa lachomwa moto Zanzibar kufutia maandamano yanaoendelea.

Kanisa lachomwa moto Zanzibar kufutia maandamano yanaoendelea.

MANDAMANO ZNZ KUZUA TAAFULANI USIKU WA KUAMKIA JANA

Sunday, May 27, 2012




Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini