Tuesday, June 5, 2012

ALI MAYAI NAYE NDANI YA WANAOTAKA UONGOZI MPYA YANGA.

Taarifa rasmi nilizozipata kutoka makao makuu ya klabu ya Yanga, ni kwamba wachezaji wawili wa zamani wa klabu hiyo Ally Mayay na Aaron Nyanda wameamua kuchukua fomu za kugombea ujumbe wa kamati ya utendaji katika uchaguzi unaokuja ndani timu hiyo.

Ally Mayay ambaye alikuwa mjumbe wa kamati hiyo kabla ya kujiuzulu baada ya kutokea kwa hali ya kutokueleweka katika uongozi uliopita, amesema yeye na Aaron wameamua kufanya hivyo baada ya kuona bado wana vitu vikubwa wanavyoweza kutoa kuisadia klabu yao kuwa katika mfumo wa kisasa utakayoiletea mafanikio timu yao.

DONE DEAL: MANCHESTER UNITED YATHIBITISHA KUMSAINI KAGAWA - VIMEBAKI VIPIMO NA KIBALI


Manchester United wamethibitisha kukamilisha usajili wa mchezaji bora wa ligi kuu ya Ujerumani Shinji Kagawa, aliyekuwa akiichezea Dortmund ambao ndio mabingwa wa Bundesliga.

Kiungo huyo mwenye miaka 23, atajiunga rasmi na United kwa ada ya £12million mwezi ujao baada ya kufaulu vipimo vya afya pamoja na kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza.

Taarifa iliyotolewa na United kupitia website yao: "Tuna furaha ya kuwatangazia kwamba tumekubaliana kimsingi na Borrussi Dortmund na Shinji Kagawa kuhamia kwenye klabu yetu.
"Dili litakamilika baada ya mchezaji kufaulu vipimo vya afya na kupata kibali cha kufanya kazi UK.
"Vitu hivi tunategemea vitakamilika ndani ya mwezi ujao."

Mchezaji wa United Rio Ferdinand alifurahishwa sana usajili wa Kagawa na akaandika kwenye ukarasa wake wa Twitter: "Karibu Manchester United Shinji Kagawa. Muda wa kupata mafanikio ni sasa kaka.!"

OFFICIAL: MANJI AJICHUKULIA FOMU YA KUGOMBEA UENYEKITI, AMCHUKULIA NA BIN KLEB YA UMAKAMU MWENYEKITI

Yusuph Manji

Muda mchache uliopita nilitoa taarifa za kuhusu Yusuph Manji kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa klabu ya Yanga, bila kuwepo kwa uthibitisho kwamba amechukua kwa ajili yake au kamchukulia mtu.
Ben Kleb akimkabidhi jezi Haruna Niyonzima
Lakini sasa kwa taarifa nilizozipata kutoka kwa mmoja ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi wa Yanga, amethibiisha kwamba Manji amejichukulia fomu mwenyewe ya kugombea uenyekiti, huku akimchukulia aliyekuwa mjumbe wa kamati ya usajili Abdallah Ahmed Bin Kleb fomu za kugombea umakamu mwenyekiti

YUSUPH MANJI ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA UENYEKITI WA YANGA.

 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa!!!!!
Taarifa rasmi na za uhakika nilizozipata kutoka makao makuu ya klabu ya Dar Young Africans ni kwamba mwanachama maarufu na tajiri wa klabu hiyo, mfanyabiashara Yusuph Mehebob Manji amechukua fomu za kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ya Yanga.

Manji ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa akiisadia Yanga kiuchumi zaidi, nusu saa iliyopita ameenda kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kuchukua fomu za uenyekiti bila kuweka wazi kama kwa ajili yake au amemchukulia mtu kwa ajili kugombea nafasi hiyo.

Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na taarifa juu ya Manji kutaka kugombea nafasi hiyo japo mwenyewe bado hajathibitisha, ingawa kitendo chake cha leo kimezidi kuupa nguvu uvumi wa kwamba anataka kugombea nafasi ya kuwa bosi wa Yanga.

Wakati huo huo taarifa nyingine zinasema kuwa aliyekuwa mjumbe Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb naye muda wowote kutoka sasa atadondoka makao ya Yanga kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea umakamu mwenyekiti.

Mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo Issac Mazwile naye ameshachukua fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.

EURO 2012: SPAIN - JE WATAWEZA KUWEKA REKODI YA KUBEBA TAJI LA TATU MFULULIZO AU WATAFUATA NYAYO ZA UFARANSA KWENYE WORLD CUP 2002?

Ufaransa ndio ilikuwa nchi ya mwisho kwenda kwenye michuano mikubwa ya kimataifa kama mabingwa wa dunia na ulaya, lakini jitihada za kuwa taifa la kwanza kushinda 'treble' makombe matatu mfululizo  katika historia ya soka la kimataifa zilishindikana kwa aibu , baada ya kumaliza kwenye nafasi ya mwisho kwenye kundi A katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002.

Spain wanajaribu kutengeneza historia kwenye kipindi hiki cha kiangazi. Ingawa maandalizi yao yamekuwa yakiwekwa kwenye wakati mgumu kutokana na majeruhi ya Carles Puyol na David Villa,  huku kukiwa na mashaka juu ya form ya Fernando Torres na hali ya kuwa fiti kwa kiungo Xavi Hernandez, kuonekana kutokuwepo kwa hatari yoyote ya kuwatokea kwa aibu ya kutolewa kwenye hatua ya makundi na kurudia historia ya aibu ya wafaransa iliyotokea miaka 10 iliyopita.

Spain kwa sasa wapo katikati ya kizazi chao cha dhahabu: wameshatengeneza na kui-master style yao ya uchezaji, kukava kila sehemu ya dimba, huku wakiwa na mazao ya vipaji vipya (Jordi Alba na wenzie) na vya zamani Xavi na kundi lake, Spain ndio ya kuogopwa zaidi kwenye michuano ya Euro.

Nahodha na golikipa Iker Casillas alisema timu yao inakumbuka sana kipigo walichopewa na Switzerland kwenye mchezo wao wa ufunguzi kwenye WOZA 2012, na sasa wamejipanga kupata suluhisho la namna ya kucheza na kupata matokeo dhidi ya timu ambazo zinapenda kupaki basi golini. Huku Italy na Ireland wakiwa ndio wapinzani wao kwenye mechi zao mbili za mwanzo katika kundi C, Spain watahitaji kupata mbinu mbadala ya kucheza dhidi ya wapaki mabasi.
Kutoka kwa Shaffihdauda.com

MBOWE:CCM IKISALIMIKA 2015 NAJIUZULU SIASA.

 
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe (pichani) amesema moto uliowashwa na chama hicho katika Operesheni Sangara utaendelea nchi nzima, lengo likiwa ni kuiondoa CCM madarakani na iwapo itasalimika mwaka 2015, atajiuzulu siasa.

Mbowe alitoa kauli hiyo juzi alipohutubia mamia ya wakazi wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wakati chama hicho kilipofanya mkutano mkubwa kwenye uwanja wa mpira wilayani humo.
Alisema CCM kimepoteza mwelekeo wa kuongoza taifa na ndiyo sababu maisha ya Watanzania yamezidi kuwa mgumu kadri miaka inavyozidi kusonga mbele.

“Wajibu wa Serikali kokote duniani ni moja tu, kuwezesha watu wake kutoka katika hali ngumu za maisha na kuwapeleka kwenye heri, leo CCM wameligawa Taifa katika vipande, wanauza rasilimali za nchi na kuwadidimiza watu wa kipato cha chini wengi wao wakiwa ni wakulima,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Ndugu zangu ngojeni niwaulize swali, wakati wa utawala wa Mwinyi na Mkapa (marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa), ni kipindi gani maisha yalikuwa mazuri?” Wananchi wakajibu (kipindi cha Mwinyi). Miaka 10 ya uongozi wa Mkapa na miaka saba ya Kikwete, ni kipindi gani maisha yamekuwa magumu zaidi?" Wakajibu (Kikwete); Je, 2015 wanakuja tena kutuomba kura huyo atakayekuja si ndiyo itakuwa mbaya zaidi, Chadema hatuwezi kukubali na moto huu tuliowasha utaendelea nchi nzima hadi Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kama CCM itasalimika nitajiuzulu siasa.”

LULU KUFIKISHWA TENA MAHAKAMANI JUNI 18

 

Mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' anayekabiliwa na kesi ya kumuua mwigizaji mwenzake, Steven Kanumba, akisindikizwa na askari Magereza kuingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa ajili ya kusomewa mashitaka  yake. Kesi hiyo imehairishwa hadi juni 18. (PICHA NA DOTTO MWAIBALE)

KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ imeahirishwa hadi Juni 18 mwaka huu,  kwa sababu upelelezi wa shauri hilo bado haujakamailika.

Wakili wa Serikali Peter Sekwao alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwa kutajwa, pia alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Baada ya kudai hivyo Hakimu Mkazi , Agustina Mmbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu, ambapo itakuja kwa kutajwa.

Awali  Mei 7 mahakama hiyo ilitupilia mbali ombi la mawakili wa upande wa  utetezi katika kesi inayomkabili Lulu kuwa mahakama
 imuone ana miaka chini ya miaka18.

MANCHESTER CITY KUMTUMA MTU KUIPELEZA STARS

Kachelo wa Man City aipeleleza Taifa Stars

Kalou wa Ivory Coast akichuana na Mwana Samatta wa Taifa Stars

MPELELEZI wa vipaji vya soka toka klabu tajiri England, Manchester City, Joe Mulberry alitua kwa siri mjini Abidjan na kupiga kambi kwenye hoteli ya Ibis Plateau, ambayo pia Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilifikia na lengo lilikuwa moja tu kuwachunguza wachezaji wa timu hiyo, Mwananchi limebaini.

Mulberry, raia wa Uingereza mwenye jukumu la kuchunguza vipaji kwa nchi za Afrika Magharibi, alifanya kazi ya kuipeleleza Stars bila kutaka mtu yeyote kufahamu kabla ya mwandishi wa habari hizi kumbaini.

Awali, Mulberry aliyeweka makazi yake nchini Ghana alipanga kwenye chumba namba 604 cha hoteli ya Ibis Plateau.

Baada ya gazeti hili kupata fursa ya kuongea naye muda mrefu, lilimbaini na ndipo naye alipomfichua siri kwamba alikuja Abidjan kwa ajili ya kuangalia pambano la Stars dhidi ya Ivory Coast.
Kwa mujibu wa uchunguzi wake wa haraka, Mulberry alivutiwa na kipaji cha mshambuliaji Mbwana Samata na cha kushangaza katika kipindi kifupi tayari alikuwa amekusanya habari zote za Samata.

Miongoni mwa dodoso muhimu alizokusanya ni pamoja na mabao mawili aliyofunga wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika dhidi ya Dynamo ya Zambia na El Merreikh ya Sudan akiwa na timu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mulberry alikiri Samata alikuwa na kipaji kikubwa lakini akataka amuone zaidi siku za usoni kujua kama alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga kama ilivyo katika kuuchezea mpira.

“Nitasafiri kwenda Ghana kumtazama kwa ajili ya pambano la ligi ya mabingwa kati ya Berekum Chelsea dhidi ya TP Mazembe pale Accra, Julai 5. Kama atakuwa yuko safi tena nitajaribu kuzungumza na timu yake.”

Hata hivyo, Mulberry alisema Samata hawezi kucheza katika Ligi Kuu ya England kwa sasa na badala yake anaweza kupelekwa katika ligi nyingine kabla ya kupata uzoefu wa kucheza ligi kubwa Ulaya. 


Wakati huohuo, msafara Taifa Stars, unatarajiwa kuwasili leo asubuhi na ndege ya Shirika la ndege la Kenya Airways ukitokea mjini Abidjan ilipocheza na kufungwa na wenyeji wao, Ivory Coast kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Stars ilitarajiwa kuondoka Abidjan jana usiku na kupitia Nairobi usiku wa manane kabla ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa moja asubuhi leo.

Kabla ya kuondoka Abidjan, kocha wa taifa Stars alikuwa ameendeleza programu yake ya mazoezi kama kawaida, huku akiwataka wachezaji wa timu hiyo wasizembee katika pambano la Jumapili dhidi ya Gambia.

Mchezaji pekee ambaye alikosekana katika mazoezi ya juzi na jana alikuwa ni mlinzi wa kushoto wa timu hiyo, Waziri Salum ambaye aliumizwa kwa bahati mbaya kifundo chake cha mguu na mlinzi mwenzake, Erasto Nyoni