Monday, June 18, 2012

BONIFACE MKWASA AJIUZULU UKOCHA TWIGA STARS

 


KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga Stars, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu leo.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba ameamua kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya na pia timu hiyo kutothaminiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mkwasa anachukua hatua hiyo, siku mbili tu tangu timu hiyo itolewe katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-1, ikifungwa 2-1 Addis Ababa na baadaye 1-0 Jumamosi mjini Dar es Salaam.
Mapema baada ya kufungwa juzi, Mkwasa alisema kwamba timu hiyo haikuwa na maandalizi mazuri na TFF haikuonekana kuijali kabisa. Lakini Mkwasa atakumbukwa mno kwa kuifikisha juu timu hiyo, akiiwezesha kushiriki fainali za Afrika miaka miwili iliyopita nchini Afrika Kusini, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.



Mkwasa
 

MAONYESHO YA ZAO LA MPUNGA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 

Waziri wa kilimo chakula na ushirika Mhe. Chiristopher Chiza.akitoa hotuba yake katika maonyesho ya zao  la mpunga yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja leo jijini Dar es salaam, ambapo amesema uzalishaji bado unakabiliwa na  changamoto mbalimbali zikiwemo,Uzalishaji na upatikanaji mdogo wa mbegu za mpunga na teknolojia bora uhifadhi na ufungashaji (Grading and packaging)(wa kwanza kulia) Naibu meya wa mansipaa ya Ilala Kheri Kessy.na wakwanza kushoto mkurungenzi msaidizi idara ya kilimo chakula na ushirika Bw.Dr Hussien Mansoor.
Mhe; Chiristopher Chiza mbele akiangalia ubora wa mbengu za mpunga alipotembelea mabanda (katikati) ni Naibu meya wa mansipaa ya ilala Kheri Kessy,(na kulia)mkurugenzi wa masoko na usambazaji wakala wa mbegu za kilimo wa Taifa (ASA)Bw;Philemon Kawamala.
Kikundi cha ngoma kijulikanacho kama Makirikiri Tanzania kilikuwa kikitoa burudani wakati wa maonyesho ya zao la mpunga leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mhe. Waziri bChiristopher Chiza (wapili kulia)akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa mkufunzi wa zana za kilimo  za kulimia zao la mpunga  Bw.Omari Issa
Waziri Chiristopher Chiza katikati, Naibu )Meya wa mansipaa ya Ilala Kheri Kessy, wa pili kutoka kustoto na mkurungenzi msaidizi Idara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dr Hussien Mansoor wakielea kutembelea mabanda ya wadau wa za mpunga,

Semina ya Viongozi wa Kidini katika kukuza Utalii

Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake katika
ufunguzi wa semina ya siku moja kwa  Viongozi wa kidini katika kukuza
dhana ya Utalii kwa wote,iliyofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani
Hotel Mjini Unguja leo,(kulia) Msahauri wa Rais masuala ya Utalii,
Issa Ahmed Othman,na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,
Said Ali Mbarouk,(kushoto) Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Ali
Halil Mirza.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Rais wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa
kidini katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote,mara baada ya kuifungua
semina ya siku moja iliyofanyika leo  katika ukumbi wa Salama Bwawani


Baadhi ya Viongozi wa madhehebu mbali
mbali ya kidini wa Mkoa wa Mjini  Magharibi wakisikiliza  kwa makini
hotuba ua ufunguzi wa  semina ya siku moja ya Viongozi wa kidini
katika kukuza dhana ya Utalii kwa wote,iliyofunguliwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo

WEMA SEPETU KUMSHUSHA NYOTA WA FILAMU OMOTOLA JALADE KUTOKA NIGERIA

Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade katika pozi matata
Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jaladekatika kivazi cha ofisini
Nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade katika kivazi cha kutokea

MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, anatarajia kumdondosha nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade hapa nchini.
Wema Sepetu, ambaye kwa sasa anatamba kwenye tasnia ya filamu anatarajia kumleta Omotola kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa filamu yake mpya iitwayo Super Star.
Filamu hiyo ya Super Star, inazungumzia maisha ya Wema kuanzia utotoni kushiriki kwake Miss Dar Indian Ocean, Miss Kinondoni, Miss Tanzania hadi kuingia kwenye filamu.
Kwenye filamu hiyo Wema ameshirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo mwimbaji wa Machozi Band, aitwaye Mwinyi.
Omotola, ambaye atatua Tanzania wiki hii, alianza kutamba kwenye tasnia hiyo baada ya kutoka na filamu iitwayo Iva mwaka 1993.
Hadi sasa nyota huyo amecheza jumla ya filamu 52, zikiwemo, Ties That Bind (2011), A Private Storm
Ije (2010), My Last Ambition (2009), Beyonce & Rihanna (2008), Temple of Justice (2008), Tomorrow Must Wait (2008) na nyingine nyingi