Thursday, May 31, 2012

MATUKIO YA UFUNGUZI WA MKUTANO WA AFDB ARUSHA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) leo mjini Arusha .
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Arusha
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka(kulia) wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .

Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipongezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dr. Donald Kaberuka (kulia) mara baada ya kumaliza kutoa hotuba ya ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha . Katikati ni Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr. Alassane Ouattara.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana mjini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (kushoto)  wakati wa sherehe za ufunguzi wa  mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) jana mjini Arusha

MKUTANO WA AFDB ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete (kulia) akisalimiana  na Waziri wa Uchumi na Fedha wa Nigeria Dr. Ngozi Okonjo- Iweala(kushoto) jana mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuwasili KIA kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa mwaka wa AFDB mjini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma jana mara baada ya kuwasilia katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA tayari kwa ajili ya kufungua mkutano wa mwaka wa AFDB mjini Arusha.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Arusha na Wizara ya Fedha wakiwa katika uwanja wa KIA wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa  mwaka wa AFDB 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete  akisalimiwa  na viongozi mbalimbali waliofika katika uwanja wa KIA jana  kwa  ajili ya kumpokea ili aende mkoani Arusha katika ufunguzi wa  mkutano wa mwaka wa AFDB mjini Arusha.