Saturday, June 9, 2012

MASHUJAA MUSICA BENDI WAZIDI KUPAA NDANI YA BUSINESS CENTRE CHINI YA UONGOZI WA CHAZ BABA.


Kiongozi na mwimbaji wa Bendi maarufu wa Mashujaa Chaz Baba jana akizikonga nyoyo za mashabiki wake kwa nyimbo zake mpya ndani ya ukumbi wa Business Centre Maeneo ya makumbusho.
Mpiga tumba maarufu Afrika Mashariki wa Bendi ya Mashujaa MCD akipafomu ndani ya Business Centre jana Usiku.


Maua ya Mashujaa Band yakiwachengua mamia ya washabiki wao ndani ya Business centre jana usiku.

CCM WAZUNGUMZIA MIRADI YA MAENDELEA JANGWANI LEO.

 Waziri wa Ujenzi Mh.John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wa wachama wa CCM Jangwani leo jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya mikakati ya chama kusikiliza kero za wananchi pamoja na mfumuko wa bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea miradi mbalimbali inayoendelea nchini
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Waziri wa uchukuzi Mh.Harrison Mwakyembe akihutubia katika mkutano wa wachama wa CCM jangwa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni mikakati ya chama  kusikiliza kero za wananchi pamoja na mfumuko ya bei na upandaji holela wa nauli na kuelezea wananchi miradi mbalimbali inayoendelea
 Katika picha kutoka kushoto ni mawaziri Prof Anna Tibaijuka, John Magufuli na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam John Guninita.
 Abdulrahman Kinana (kulia) akipeana  mkono na waziri John Magufuli kushoto.

 Wanachama wa CCM wakichambua baadhi ya kadi ya vyama pinzani zilizorudishwa na wanachama wao kama zinavyoonekana katika picha
 Waziri wa nyumba na maendeleo na makazi Profesa Anna Tibaijuka akifafanua jambo katika mkutano huo
Viongozi wa CCM pamoja na mawaziri wakiimba katika mkutano huo uliofanyika Jangwani jijini Dar es salaam leo

NBC YADHAMINI MKUTANO WA CRB.

 

Meneja Mahusiano  wa NBC, Danstan Kolimba akitoa mada kuhusu ni
jinsi gani sekta ya ujenzi inavyoweza kunufaika na huduma za benki
hiyo katika Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Makandarasi (CRB) uliofanyika
jijini Dar es Salaam jana.  NBC ilidhamini mkutano huo.
Meneja Mahusiano  wa NBC, Danstan Kolimba (kulia) pamoja na baadhi
ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Makandarasi (CRB)
uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.  NBC ilidhamini mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Makandarazi
wakimsikiliza Meneja Mahusiano wa NBC, Danstan Kolimba (hayupo
pichani) wakati akitoa mada yake kuhusu jinsi sekta ya ujenzi
inavyoweza kunufaika na huduma zitolewazo na NBC  wakati wa mkutano
huo uliodhaminiwa na NBC jijini Dar es Salaam jana

PINDA AFUNGUA KIWANDA CHA NYUKI KIBAHA NA AMTEMBELEA MBUNGE ROMBO MOI


 



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini Juni 9,2012 ambaye amehamishiwa katika hospitali ya tiba ya mifupa ya MOI katika hospitali ya Tafa ya Muhimbili akitokea hospitali ya KCMC Moshi kwa matibabu zaidi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mitambo baada ya kufunguza kiwanda cha kusindika asali cha  Organic Honey katika kijiji cha Visiga  mkoani Pwani  kinachomilikiwa na Kampuni ya  Boleyn  International, Juni 9, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI WA HABARI FENELLA MUKANGALA ATEMBELEA TWIGA STARS KAMBINI JKT RUVU.


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mkangalla akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Kambi ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) cha Ruvu Meja Alex Kakwaya wakati alipokwenda kutembelea kikosi cha Timu ya Tiwiga Stars kinayotarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopiia. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mkangalla akisalimiana na mmoja wa Kamanda wa kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa cha Ruvu JKT wakati alipokwenda kutembelea kikosi cha Timu ya Tiwiga Stars kinayotarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopiia. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenela Mkangalla akiteta  jambo na  Kaimu Kamanda wa Kambi ya Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) cha Ruvu Meja Alex Kakwaya wakati alipokwenda kutembelea kikosi cha Timu ya Twiga Stars kinachotarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na timu ya Ethiopiia. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).