Friday, June 8, 2012

HEKAHEKA YA USAJILI YANGA KUFURU MWAKA HUU MAXIMO ATUA JUMA 4 KUZUNGUMZA NAO.

Baada ya kufanya vibaya katika msimu uliopita, Yanga wameendelea kuunda timu upya, baada ya juzi kumsainisha Kelvin Yondan, leo hii timu hiyo imehamia kwenye benchi la ufundi.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya zinasema klabu hiyo imemtumia tiketi ya ndege kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Marcio Maximo kwa ajili ya kuja kufanya mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo kwa ajili ya kuliongoza benchi la ufundi la wanajangwani kuanzia msimu ujao.

"Mpaka sasa tumefanya mazungumzo ya awali na Maximo na tumefikia makubaliano ya kimsingi, ambayo tunaweza kuja kuyakamilisha hapa nchini atakapotua siku ya jumanne wiki ijayo." - kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WAWILI NA KAMISHNA WA TUME UTUMISHI WA MAHAKAMA.

 


Rais Dkt JAKAYA KIKWETE akimwapisha SEMISTOCLES KAIJAGE (kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Kabla ya uteuzi huo KAIJAGE alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam.

Jaji wa Mahakama ya Rufani MUSSA KIPENKA akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais  Dkt JAKAYA KIKWETE Ikulu jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania MOHAMMED CHANDE OTHMAN.

Rais JAKAYA KIKWETE akimwapisha EDWARD RUTAKANGWA kuwa kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dares Salaam.

PRESIDENT KIKWETE MEETS VODACOM GROUP CHAIRMAN-PETER MOYO.


 

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with VODACOM group Chairman Mr.Peter Moyo at Dar es Salaam State House this morning when the later paid a courtesy call on him.

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets VODACOM  group delegation led by its chairman Mr.Peter Moyo(Third left) at Dar es Salaam State House this afternoon. Others in the picture are from left, Chief Officer Corporate Affairs Ms.Mwamvita Makamba, and  VODACOM Managing Director Mr. Rene Meza(Second left)(Photos by Freddy Maro).

TETESI HAI:HATARI SIMBA,"BAADA YA YONDAN SASA NI OKWI.

 

Sekeseke la usajili limeendelea kupamba moto.

Katika kuhakikisha wanaibomoa kabisa safu ya ushambuliaji wa watani wao Dar-young African katika mechi ya kufunga msimu uliopita. Klabu hiyo bingwa ya afrika mashariki na kati, Dar Young Africans inakaribia kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda na tegemeo la klabu ya Simba, Emmanuel Okwi.

Taarifa za udaku nilizozipata kutoka ndani ya Yanga ni kwamba timu yao ipo tayari kulipa fedha wanazozitaka Simba ili kuweza kupata huduma za Okwi msimu ujao. Taarifa zinasema kwamba Okwi ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda anatarajiwa kutua Tanzania ndani ya kipindi cha masaa 72 kuja kumaliza suala la usajili wake kwenda Yanga ambao inasemekana wamemuhaidi fedha nyngi sana.

GAMBIA WAKIWA MAZOEZINI KATIKA UWANJA WA KARUME JIJINI DAR-ES-SALAAM,TAYARI KUIVAA STARS JUMAPILI KATIKA MCHEZO WA KUWANIA KUFUZU KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2014 BLAZIL.


Timu ya Gambia ikiwa mazoezini katika uwanja wa karume jijini dar es salaam jioni hii kwa ajili ya mechi ya Timu ya Taifa Star katika uwanja wa Taifa jumapili  jijini dar es salaam.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Wachezaji wa timu hiyo wakijifua kwa kuchezea mpira wa pasi fupifupi kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam leo jioni