Monday, June 4, 2012

MKUU WA WILAYA ATAKA UONGOZI YANGA

 

MKUU wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu pamoja na mwanachama wa klabu ya Yanga Abdallah Binkleb jana wamechukua fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe katika uchaguzi wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika Julai 15. 
Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga  Francis Kaswahili kuchukua fomu kwa wanachama hao kunafanya idadi ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu hiyo kufikia  10 .
Mbali na hao wanachama wengine waliochukua fomu ni pamoja na John Jambele anayewania uenyekiti, huku Ayoub Nyenzi akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti. 
“Waliochukua fomu kuwania ujumbe wa kamati ya Utendaji mbali na Muhingo na Binkleb  ni  Isack Chandi, Jumanne Mwamwenye na Salehe Hassan,”.

ZOEZI LA UCHUKUAJI FOMU YANGA LADODA

ZOEZI la uchukuaji fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Yanga limedoda baada ya wanachama wachache kujitokeza.
Zoezi hilo lililoanza juzi hadi kufikia jana ni wagombea sita tu ndio waliojitokeza kuchukua fomu hizo ambapo kati yao ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Zoezi hilo litakomea juni 6 kabla ya uchaguzi huo ambao ni wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi ukipangwa kufanyika Julai 15

SUGU AKUMBUSHIA ENZI ZAKE DAR LIVE JUMAPILI.

 
Msanii wa HIP HOP ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Mr II' juzi alizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kwa kufanya makamuzi katika tamasha la Usiku wa Sugu. Sugu alisindikizwa na Juma Nature, Profesa Jay, Vinega, Mkoloni na wengineo wengi kwenye shoo hiyo iliyokuwa ya aina yake.
Katika picha juu Sugu akiwarusha mashabiki ndani ya Dar Live .
Sugu na Mkoloni kazini.
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari nae akitoa 'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.
Profesa Jay akiwapa burudani mashabiki wa Dar Live.
Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi likifanya makamuzi stejini.
Suma G nae alikuwepo kuupamba usiku huo.
Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wa Dar Live.
Nyomi iliyohudhuria Usiku wa Sugu.
Baadhi ya mashabiki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sugu

MBUNGE WA BAHI APANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU JANA.

Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omary Badwel (CCM), akisindikizwa na askari polisi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, baada ya kusomewawa mashitaka akituhumiwa kushawishi na kupokea rushwa ya sh. milioni 1. Kesi hiyo imehairishwa hadi juni 18 mwaka huu. (PICHA NA PHILEMON SOLOMON)
Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omary Badwel (CCM), akisindikizwa na askari polisi kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana.

TWANGA PEPETA WAACHIA NYIMBO MPYA,WATAMBULISHA PIA KIKOSI KAZI KIPYA.

 

 Mkurugenzi wa  ASET Asha Baraka akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mango asubuhi hii wakati alipotangaza kikosi kamili cha bendi hiyo na wimbo mpya wa bendi hiyo leo, kushoto ni mwanamuziki wa bendi hiyo Saleh Kupaza.

 Wanenguaji wa kike wa bendi hiyo wakifanya vitu vyao mbele ya waandishi wa habari.
  Rapa wa bendi hiyo J4 akifanya vitu vyake jukwaani huku wanenguaji wa kiume wa bendi hiyo wakitoa burudani mbele ya waandishi wa habari.

SERIKALI YA NIGERIA YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KUFUATIA AJALI YA NDEGE ILIYOSABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU150.

Siku tatu za maombolezi ya kitaifa zimetangazwa kuanzia leo nchini Nigeria kufuatia ajali ya ndege ambapo zaidi ya 150 walikufa.
Ndege hiyo aina ya Boeing MD-83 iliangukia eneo moja la kuchapisha karatasi na makazi mjini Lagos kabla ya kulipuka. Vikosi vya waokoaji vipo eneo hilo usiku kucha.
Taarifa zinasema abiria wote katika ndege hiyo walikufa. Hakuna majeruhi katika eneo la ajali japo haijabainika rasmi ni watu wangapi ambao wamekufa.
Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Dana Air ambayo hutoa huduma zake kati ya mji wa Abuja na Lagos. Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Iju Kaskazini mwa uwanja wa ndege.
Rais Goodluck Jonathan ameamrisha kufanyika uchunguzi kamili kubainisha chanzo cha ajali hiyo.
Mwandishi wa BBC Mjini Lagos Will Ross amesema hapo mwezi Mei ndege nyingine inayomilikiwa na kampuni ya Dana Air ilipata hitilafu za mitambo na kulazimika kutua ghafla.
Nigeria kama nchi nyingi Barani Afrika inakumbwa na matatizo ya usalama wa safari za anga.
Hata hivyo kumekuwa na juhudi za kuboresha safari za anga tangu kutokea misururu ya ajali za ndege mwaka 2005

Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Sothern Sudan katika mashindano ya Miss East Africa 2012

Mrembo huyo ni  Miss Akuot Philip Suzan (20)  mwenye urefu wa futi 6.1 anaekaa Juba, Sudan  ni mwanamitindo Nchini humo na anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha makelele Nchini Uganda mwaka huu.

Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss Ayisha Nagudi (23) ambae ni mwakilishi wa Uganda.

Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ambayo yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.

Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa.

Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania.

Miss Akuot Philip Suzan (20) katika pozi