Monday, June 4, 2012

MKUU WA WILAYA ATAKA UONGOZI YANGA

 

MKUU wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu pamoja na mwanachama wa klabu ya Yanga Abdallah Binkleb jana wamechukua fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe katika uchaguzi wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika Julai 15. 
Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga  Francis Kaswahili kuchukua fomu kwa wanachama hao kunafanya idadi ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu hiyo kufikia  10 .
Mbali na hao wanachama wengine waliochukua fomu ni pamoja na John Jambele anayewania uenyekiti, huku Ayoub Nyenzi akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti. 
“Waliochukua fomu kuwania ujumbe wa kamati ya Utendaji mbali na Muhingo na Binkleb  ni  Isack Chandi, Jumanne Mwamwenye na Salehe Hassan,”.

ZOEZI LA UCHUKUAJI FOMU YANGA LADODA

ZOEZI la uchukuaji fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Yanga limedoda baada ya wanachama wachache kujitokeza.
Zoezi hilo lililoanza juzi hadi kufikia jana ni wagombea sita tu ndio waliojitokeza kuchukua fomu hizo ambapo kati yao ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Zoezi hilo litakomea juni 6 kabla ya uchaguzi huo ambao ni wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi ukipangwa kufanyika Julai 15

No comments:

Post a Comment