Tuesday, May 29, 2012

ALIYEKUWA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA WA ZAMANI, IDD SIMBA AFIKISHWA MAHAKAMA LEO NA WENZAKE 3

ALIYEKUWA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA WA ZAMANI, IDD SIMBA AFIKISHWA MAHAKAMA LEO NA WENZAKE 3

 Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa zamani, Idd Simba akiongozwa na askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashata 8 likiwemo la kula njama na, kughushi pamoja na kulitia hasara Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA zaidi ya Sh. milioni 300. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengeni watatu.
 Wakili Said Hamad El-Maamry (kushoto) akizungumza na Idd Simba Mahakamani hapo.
Mmoja wa watuhumiwa katika kesi hiyo, Aliyekuwa Diwani wa Sinza, Salim Mwaking'nda akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mchana.

Na Mwandishi Wetu
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya awamu ya Pili, Idd Simba ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la UDA leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashata 8 likiwemo la kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na kulisababishia hasara Shirika hilo ya zaidi ya Sh. bilioni 2.3

 Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengine watatu ambao Mbali na Idd Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ,wengine ni Mkurugenzi Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo, Victor Milanzi wa shirika hilo ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa na Said El Mamry ambapo upande wa Jamhuri unawakilishwa na wakili wa Taasisis ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,Ben Lincol.

ANGETILE OSIAH ANG'ATUKA YANGA SC

 


KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah ametangaza kujivua nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya Yanga.
 Osiah amesema kuwa  analazimika kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za shirikisho hilo na atawasilisha barua kwa katibu mkuu wa Yanga, Mwesiga Selestine. 
Alisema kuwa licha ya kuteuliwa muda mrefu kushika wadhifa wa ukatibu wa TFF, alishindwa kuwasilisha barua ya kujitoa katika kamati ya uchaguzi kutokana na kuingwa na majukumu ndani ya shirikisho hilo
“Nimelazimika kufanya hivyo kwani kwa sasa Yanga inahitaji kufanya uchaguzi mdogo kwa lengo la kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi walioachia ngazi Yanga hivyo inabidi nafasi yangu ijazwe ili kamati iweze kuendesha mchakato wake kikamilifu,”alisema. 
TFF kupitia kamati ya uchahizi iliyo chini ya mwenyekiti wake Deogratius Lyato iliiagiza kamati ya uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Jaji John Mkwawa ifanye uchaguzi wake kuziba nafasi za nane za viongozi waliojiuzulu na mjumbe mmoja aliyefariki dunia. 
Hatua hiyo inafuati hivi karibuni kujiuzulu kwa mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga kutokana na shinikizo la baadhi ya wanachama wakiongozwa na baraza la Wazee waliomtaka kufanya hivyo kwa madai ya kutoiletea mafanikio klabu na hatimaye kupokwa ubingwa wao wa ligi kuu bara ulioenda kwa Simba na wao kuishia nafasi ya tatu. 
Awali makamu mwenyekiti wa Yanga Davis Mosha alitangaza kujiengua katika uongozi miezi michache baada ya kuchaguliwa kwa madai ya kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe wa kamati ya utendaji, Theonest Rutashoborwa alifariki dunia. 
Kama hiyo haitoshi, wajumbe wengine walioachia ngazi Yanga ni pamoja na Seif Ahmed, Mbaraka Igangula, Mzee Yusuf, Ally Mayay, Charles Mgondo  na Mohammed Bhinda

UKRAINE, CROATIA WATAJA VIKOSI VYA UBINGWA

KIKOSI KAMILI CHA CROATIA:
MAKIPA: Stipe Pletikosa (FC Rostov), Ivan Kelava (GNK Dinamo Zagreb), Danijel Subašić (AS Monaco FC).
MABEKI: Jurica Buljat (Maccabi Haifa FC), Vedran Ćorluka (Tottenham Hotspur FC), Danijel Pranjić (FC Bayern München), Gordon Schildenfeld (Eintracht Frankfurt), Josip Šimunić (GNK Dinamo Zagreb), Darijo Srna (FC Shakhtar Donetsk), Ivan Strinić (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Domagoj Vida (GNK Dinamo Zagreb).
VIUNGO: Milan Badelj (GNK Dinamo Zagreb), Tomislav Dujmović (FC Dinamo Moskva), Ivo Iličević (Hamburger SV), Niko Kranjčar (Tottenham Hotspur FC), Luka Modrić (Tottenham Hotspur FC), Ivan Perišić (Borussia Dortmund), Ivan Rakitić (Sevilla FC), Ognjen Vukojević (FC Dynamo Kyiv).
WASHAMBULIAJI: Eduardo (FC Shakhtar Donetsk), Nikica Jelavić (Everton FC), Mario Mandžukić (VfL Wolfsburg), Ivica Olić (VfL Wolfsburg).

Kocha wa Ukraine, Oleg Blokhin


KIKOSI KAMILI UKRAINE
MAKIPA: Oleksandr Goryainov (FC Metalist Kharkiv), Maxym Koval (FC Dynamo Kyiv), Andriy Pyatov (FC Shakhtar Donetsk).
MABEKI: Bohdan Butko (FC Illychivets Mariupil), Olexandr Kucher (FC Shakhtar Donetsk), Taras Mikhalik (FC Dynamo Kyiv), Yaroslav Rakitskiy (FC Shakhtar Donetsk), Yevhen Selin (FC Vorskla Poltava), Yevhen Khacheridi (FC Dynamo Kyiv), Vyacheslav Shevchuk (FC Shakhtar Donetsk).
VIUNGO: Olexandr Aliyev (FC Dynamo Kyiv), Denys Garmash (FC Dynamo Kyiv), Oleh Gusev (FC Dynamo Kyiv), Yevhen Konoplyanka (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Serhiy Nazarenko (SC Tavriya Simferopol), Ruslan Rotan (FC Dnipro Dnipropetrovsk), Anatoliy Tymoshchuk (FC Bayern München), Andriy Yarmolenko (FC Dynamo Kyiv).
WASHAMBULIAJI: Andriy Voronin (FC Dinamo Moskva), Marko Dević (FC Metalist Kharkiv), Artem Milevskiy (FC Dynamo Kyiv), Yevhen Seleznyov (FC Shakhtar Donetsk), Andriy Shevchenko (FC Dynamo kyiv

CUF YAWATAKA WAFUASI WAKE NA WANANCHI ZANZIBAR KUWA WATULIVU, WAVUMILIVU NA KUTOA MAWAZO YAO BILA JAZBA

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar

Chama cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.

Taraifa ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mawazo yao”

Taarifa hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa Kizanzibari.

KOCHA IVORY COAST ATIMULIWA KAZI SIKU CHACHE KABLA YA KUIVAA STARS

ZIKIWA zimesalia siku nne kabla ya kumenyana na timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Kocha wa Ivory Coast Francois Zahoui ametimuliwa kazi. Stars inatarajiwa kusafiri keshokutwa kuelekea Abidjani kwa ajili ya kumenyana na Ivory Coast katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe Dunia itakayochezwa Juni 2.

Habari kutoka Ivory Coast zilisema jana Shirikisho la Soka la nchi hiyo (FIF) limemfuta kazi kocha huyo saa 24 baada ya timu yake kunyukwa mabao 2-1 na Mali katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Ufaransa.


Mchezaji wa zamani wa Ufaransa Sabri Lamouchi ndio ametangazwa kuwa kocha mpya wa Tembo hao ambaye ataiongoza timu hiyo katika mechi za kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 pamoja na ile ya Kombe la Mataifa Afrika 2013.


Uteuzi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 ambaye amewahi kuwa kiungo wa Auxerre, Monaco, Inter na Marseille umeshtua wengi kwasababu hakuwa kwenye orodha ya waliokuwa wakitarajiwa kuchukua nafasi hiyo kama ilivyokuwa kwa kocha wa zamani wa Senegal Bruno Metsu, Eli Baup, Antoine Kombouaré na kocha wa zamani wa England Sven Goran Eriksson.


Lamouchi alistaafu kucheza soka ya kimataifa mwaka 2001 baada ya kucheza mechi 12 tu dhidi ya Les Bleues na kufunga bao moja, hajawahi kuifundisha timu yoyote ya taifa.

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA


Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo na UwaGeneral Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akitoa heshima zake.  wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani  Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei. Picha zote na MO BLOG
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim  akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua kama ishara ya kuwakumbuka walinda Amani wa Afrika.

ZIARA YA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR KATIKA KANISA LILILOCHOMWA MOTO


-Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
-Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.
Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini

SPRITE YADHAMINI KLINIKI YA KIKAPU (Zaidi ya vijana 200 kushiriki)

Mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu na anyechezea ligi ya NBA ya Marekani , Hasheem Thabeet akiongea  na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu kliniki ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Sprite itakayofanyika katika viwanja vya Don Bosco, Upanga Dar es Salaam kuanzia Ijumaa Juni Mosi 2012.
Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Maluwe akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani)kuhusu ya kliniki ya vijanai chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika katika viwanja vya Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia Ijumaa Juni Mosi mwaka huu. Kliniki hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola kupitia kinywaji cha Sprite. Katikati ni mchezaji wa Ligi maarufu duniani ya NBA  Hasheem Thabeet na kulia ni Meneja Bidhaa Msaidizi wa Coca-Cola Tanzania Warda Kimaro.
 

THOMAS ULIMWENGU KUTOENDA KUWAVAA AKINA KOLO TOURE

Zikiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya timu ya Taifa ya Tanzania kusafiri kwenda kuwavaa Ivory Coast - taarifa rasmi kutoka kambi ya timu hiyo zinasema kwamba mshambuliaji Tom Ulimwengu hatosafiri na timu hiyo. 

Ulimwengu, mshambuliaji chipukizi wa timu ya soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ameshindwa kupona maumivu ya kifundo cha mguu aliyopata akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Mbali na Ulimwengu Taifa Stars pia itakuwa bila ya kiungo wa kutumainiwa wa Yanga Nurdin Bakari ambaye pia ameshindwa kupona maumivu ya nyama za paja yaliyokuwa yanamkabili. Ulimwengu na Nurdin wote walikosa mchezo wa kirafiki ulioisha kwa sare ya bila kufungana dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi uliochezwa Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita.