Tuesday, May 29, 2012

CUF YAWATAKA WAFUASI WAKE NA WANANCHI ZANZIBAR KUWA WATULIVU, WAVUMILIVU NA KUTOA MAWAZO YAO BILA JAZBA

Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na katibu Mkuu wa chama cha CUF Maalim Seif Sharif Hamad.
 
Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar

Chama cha Wananchi(CUF) kimewataka wananchi kutulia na Serikali kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar.

Taraifa ya Chama hicho kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Mkurugenzi wa Uenezi na Mahusiano na Umma,Salim Bimani ilisema “Chama cha CUF kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila jazba na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mawazo yao”

Taarifa hiyo ilisema kwamba vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa moto na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa Kizanzibari.

No comments:

Post a Comment