Monday, June 4, 2012

SERIKALI YA NIGERIA YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KUFUATIA AJALI YA NDEGE ILIYOSABABISHA VIFO VYA ZAIDI YA WATU150.

Siku tatu za maombolezi ya kitaifa zimetangazwa kuanzia leo nchini Nigeria kufuatia ajali ya ndege ambapo zaidi ya 150 walikufa.
Ndege hiyo aina ya Boeing MD-83 iliangukia eneo moja la kuchapisha karatasi na makazi mjini Lagos kabla ya kulipuka. Vikosi vya waokoaji vipo eneo hilo usiku kucha.
Taarifa zinasema abiria wote katika ndege hiyo walikufa. Hakuna majeruhi katika eneo la ajali japo haijabainika rasmi ni watu wangapi ambao wamekufa.
Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Dana Air ambayo hutoa huduma zake kati ya mji wa Abuja na Lagos. Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Iju Kaskazini mwa uwanja wa ndege.
Rais Goodluck Jonathan ameamrisha kufanyika uchunguzi kamili kubainisha chanzo cha ajali hiyo.
Mwandishi wa BBC Mjini Lagos Will Ross amesema hapo mwezi Mei ndege nyingine inayomilikiwa na kampuni ya Dana Air ilipata hitilafu za mitambo na kulazimika kutua ghafla.
Nigeria kama nchi nyingi Barani Afrika inakumbwa na matatizo ya usalama wa safari za anga.
Hata hivyo kumekuwa na juhudi za kuboresha safari za anga tangu kutokea misururu ya ajali za ndege mwaka 2005

No comments:

Post a Comment