Friday, June 8, 2012

TETESI HAI:HATARI SIMBA,"BAADA YA YONDAN SASA NI OKWI.

 

Sekeseke la usajili limeendelea kupamba moto.

Katika kuhakikisha wanaibomoa kabisa safu ya ushambuliaji wa watani wao Dar-young African katika mechi ya kufunga msimu uliopita. Klabu hiyo bingwa ya afrika mashariki na kati, Dar Young Africans inakaribia kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda na tegemeo la klabu ya Simba, Emmanuel Okwi.

Taarifa za udaku nilizozipata kutoka ndani ya Yanga ni kwamba timu yao ipo tayari kulipa fedha wanazozitaka Simba ili kuweza kupata huduma za Okwi msimu ujao. Taarifa zinasema kwamba Okwi ambaye kwa sasa yupo nchini Uganda anatarajiwa kutua Tanzania ndani ya kipindi cha masaa 72 kuja kumaliza suala la usajili wake kwenda Yanga ambao inasemekana wamemuhaidi fedha nyngi sana.

No comments:

Post a Comment