Thursday, May 31, 2012

MKUTANO WA AFDB ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete (kulia) akisalimiana  na Waziri wa Uchumi na Fedha wa Nigeria Dr. Ngozi Okonjo- Iweala(kushoto) jana mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuwasili KIA kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa mwaka wa AFDB mjini Arusha.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma jana mara baada ya kuwasilia katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA tayari kwa ajili ya kufungua mkutano wa mwaka wa AFDB mjini Arusha.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Mkoa wa Arusha na Wizara ya Fedha wakiwa katika uwanja wa KIA wakimsubiri Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa  mwaka wa AFDB 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete  akisalimiwa  na viongozi mbalimbali waliofika katika uwanja wa KIA jana  kwa  ajili ya kumpokea ili aende mkoani Arusha katika ufunguzi wa  mkutano wa mwaka wa AFDB mjini Arusha.

No comments:

Post a Comment