Saturday, June 23, 2012

OKWI AGEUKA LULU SOKO LA USAJILI: BAADA YA ORLANDO, SASA TIMU YA SERIE A NA MAMELOD SUNDOWNS ZAGOMBEA SAINI YAKE

 

Nyota ya jaa ya mshambuliaji wa kimataifa wa Simba na Uganda Emmanuel Okwi, inazidi kuwaka, siku chache baada ya klabu bingwa ya Orlando Pirates kutuma barua ya kutaka mshambuliaji huyo wa Simba aende kufanya majaribio kwenye klabu hiyo, leo hii timu pinzani ya Orlando kwenye ligi ya Afrika kusini, Mamelodi Sundowns wameuambia uongozi wa Simba kwamba wapo tayari kumnunua mshambuliaji huyo.

Taarifa zilizothibitishwa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinasema kwamba Mamelodi wametuma maombi ya kutaka kumsaini Okwi ambaye amekuwa na msimu mzuri sana ndani na nje ya ligi kuu ya Vodacom msimu ulioisha.

Pia chanzo changu hicho cha habari kutoka ndani ya Simba kilisema kwamba kuna timu moja inayoshiriki ligi kuu ya Italia Serie A, wameonyesha nia ya kumtaka Okwi lakini wamesema kwamba wanasubiri mpaka michuano ya Euro itakapoisha ndipo watakapoamua juu ya suala la usajili wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda.

No comments:

Post a Comment