Friday, June 1, 2012

BREAKING NEWS: SIMBA KUMTEMA MACHAKU


 
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Salum Machaku pichani anaweza kutolewa kwa mkopo kwa nusu msimu, ili ajifundishe adabu- kwani hivi sasa mabega yamepanda mno juu.
 
Habari ambazo zimepatikana kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Machaku amekuwa akijisikia mno baada ya kufanya vizuri kidogo msimu huu akiwa na jezi ya Wekundu wa Msimbazi, kiasi kwamba amekuwa akidharau hadi viongozi.
Kiongozi mmoja wa juu wa Simba,alisema kwamba uongozi ulifanya jitihada kubwa za kumbadili kitabia Machaku, ikiwemo kumuweka chini ya mchezaji anayeogopwa na wachezaji wote, Haruna Moshi ‘Boban’, lakini ikashindikana.
“Sasa tunataka tumpe nafasi ya mwisho, tumpeleke kwa mkopo klabu nyingine akacheze  mzunguko mmoja tu, akijirekebisha, tunamrudisha, ikishindikana ndio imetoka,”alisema kiongozi huyo.
Wakati huo huo, Machaku ni kati ya wachezaji ambao wamo kwenye orodha ya nyota wanaotakiwa na mahasimu wa jadi wa Simba, Yanga. Na katika siku za karibuni, Machaku amekuwa karibu mno na kipa wa Yanga, Shaaban Hassan Kado ambaye waliwahi kucheza naye pamoja Mtibwa Sugar na timu ya taifa

No comments:

Post a Comment