Saturday, June 16, 2012

EDDA MISS KIGAMBONI CITY 2012.



Redds Miss Kigamboni City  2012 , Edda Sylvester (21) akipunga mono kwa furaha mara baada ya kutangazwa mshindi na kuvikwa taji la Kigamboni City katika shindano lililofanyika katika Ukumbi wa Navy Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Mroki Mroki) 

Warembo walioingia hatua ya tano bora ya Miss Kigamboni 2012, kutoka kulia Elizabeth Boniface, Ester Albert, Edna Sylvester, Hadija Kombo na Agnes Goodluck wakipozi kwa picha jukwaani baada ya kutajwa kuvuka nafasi hiyo na kupata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 baadea mwaka huu.

Warembo waliokuwa wakiwania taji la Miss Kigamboni City 2012 wakicheza show ya ufunguzi jukwaani.

Redds Miss Kigamboni City  2012 , Edda Sylvester (katikati) akiwa na mshindi wa pili Agnes Goodluck (kushoto) na mshindi wa tatu Elizabeth Boniphace mara baada ya kutangwazwa washindi. Edda aliwashinda warembo wengine 9 katika shindano hilo.

No comments:

Post a Comment