Wednesday, June 13, 2012

PODOLSKI NA MULLER WALIFELI DHIDI YA URENO: JE REUS NA SCHURRLE WATAANZA DHIDI YA UHOLANZI.

Mchezo wao kwanza wa Euro 2012 ulienda kwa mujibu wa Ujerumani walivyotaka - kwa upande wa matokeo, lakini vijana wa Joachim Low hawakuonyesha uwezo mkubwa ambao wengi walikuwa wakiutegemea dhidi ya Ureno. Ushindi wa 1-0 ulikuwa ni bahati kwa timu hiyo kwa kuwa hata Ureno walipoteza sana nafasi kwa kutokuwa na bahati waliyoipata Ujerumani.

Ndio maana haishangazi kuona umma wa Ujerumani ukitegemea kuona mabadiliko kwenye mechi zijazo, kwa kuwa hawakuona timu yao ikicheza kwa kutengeneza nafasi nyingi za magoli dhidi ya kikosi cha Paulo Bento. Low alifanya uamzui mkubwa kwa kumchezesha Mats Hummels na Mario Gomez, lakini mashabiki wanataka kocha wao aongezee ujasiri wakati wa mechi zijazo.

Kuna maswali juu ya nafasi mbili: Thomas Muller na Lukas Podolski wote wanaweza wakaanzia benchi kwenye mechi zijazo. Wote walionyesha kwamba wapo tayari kucheza kwa kujituma bila kuchoka lakini kiukweli hawakucheza vizuri, na sasa Marco Reus na Andre Schurrle wanaweza kuwa wabadili wao dhidi Uholanzi?

Akiwa mmoja ya chipukizi bora wa ligi ya Ujerumani msimu uliopita, kiwango cha Marco Reus akiwa Borussia Monchengladbach kimeonyesha ubora anaoweza kuuleta ndani ya kikosi: akiwa na na rekodi nzuri za ufungaji na ubunifu mzuri kiwanjani. Kwa upande wa Schurrle amekuwa katika form nzuri kwa siku za hivi karibuni katika mechi za kirafiki kuelekea kwenye Euro, pia alikuwa na msimu mzuri na Bayern Leverkusen, na hakuna ubishi kwamba amaelata maswali mengi juu ya nani aanze kati yake na Podolski.

No comments:

Post a Comment