Thursday, June 7, 2012

"SITAKI UBABAISHAJI ATCL,ATAKAECHUKIZWA NA UAMUZI WANGU NA YEYE ATOKE-MWAKYEMBE"

Waziri wa uchukuzi Dr HARISON MWAKYEMBE,hii leo ameuelezea umma vigezo alivyotumia kumsimamisha kazi aliyekuwa Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege la Serikali ATCL Bw.Paul Chizi,kuwa ni utendaji mbovu ikiwa ni pamoja na Shirika hilo kuwapeleka maofisa wawili wa ATCL kusimamia zoezi la kushona sare 17 za wafanyakazi wa Shirika hilo Nchini China  kwa siku zaidi ya 45, ambapo walikuwa wakilipwa posho ya kukaa huko kila siku.Kigezo kingine ni kutokuwa na mipango thabiti ya kulifanya Shirika hilo kuwa la kujitegemea badala ya kubaki chini ya Serikali kila uchao. 
Mwakyembe ameonesha kushangazwa na baadhi ya waandishi wa habari nchini kukurupuka na kulitolea maoni suala hilo kinyume na hali halisi ilivyo

No comments:

Post a Comment