Monday, July 16, 2012

MANCHESTER UNITED NDIO MABINGWA WA SERENGETI FIESTA BONANZA DSM

 

Ilao Ejakait Meneja wa Uendeshaji upande wa mauzo kampuni ya bia ya Serengeti akikabidhi zawadi kombe kapteni wa timu ya mashabiki wa klabu ya Manchester United ya Uingereza katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza lililofanyika jana kwenye viwanja vya Sigara TCC Chang'ombe jijini Dar es salaam ,baada ya timu ya mashabiki hao kuwafunga mashabiki wa timu ya Bacelona na kuchukua kombe hilo Bonanza hilo lilishirikisha mashabiki wa vilabu mbalimbali vya Ulaya, katikati ni Allan Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager na kulia ni Bahati Singh Joseph Mahawi meneja Mauzo wa Serengeti
;
Kapten wa timu ya mashabiki wa Manchester United akinyanyua juu juu kombe lao mara baada ya timu ya mashabiki hao kuwafunga mashabiki wa timu ya Bacelona na kuchukua kombe hilo kulia ni Ilao Ejakait Meneja Uendeshaji na  mauzo  kampuni ya bia ya Serengeti Allan  Chonjo Meneja wa bia ya Serengeti Lager
Mashabiki wa Manchester United wakishangilia kwa nguvu baada ya kukabidhiwa kombe lao.

Meneja mauzo wa kampuni ya bia ya Serengeti Joseph Mahawi akikabidhi kombe la mshindi wa pili timu ya mashabiki wa Barcelona jana kwa kapten wa timu hiyo Michael Mashoto mara baada ya kuchukua nafasi ya pili katika bonanza la Serengeti Fiesta Soccer Bonanza kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe kwa kufungwa na Manchester United
Mashabiki wa Manchester United wakishangilia baada ya kuingia fainali.
Mashabiki wa Machester United wakiimba kwa furaha
Warembbo wa Chelsea walikuwepo kuwakilisha
Wachezaji wa timu za mashabiki wa Manchester United na Barcelona wakichuana vikali katika mchezo wao wa fainali ambapo Manchester United ilishinda mchezo huo.
Mchuano mkali ukiendelea kwenye viwanja vya TCC Sigara.
Mambo ya mnyama na burudani ileile
Vinywaji vilikuwa vya kutosha kama vinavyoonekana katika picha
Mashabiki wa timu ya Chelsea wakishangilia mara baada ya kuingia nusu fainali.
Wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kiko sawa kutoka kulia ni Kaisi, Bahati Singh Meneja Matukio na Promosheni Queen Sendiga Afisa wa Promosheni Kanda ya Dar es salaam na Ilao Ejakait Meneja wa Uendeshaji upande wa mauzo
Mdau Heavy D. akiwa amekaa chini hoi huku jua likimpiga vibaya baada ya kukata tamaa kabisa kutokana na timu yake ya Arsenal kutolewa mapema katika bonanza hilo hapa anaonekana kama vile analalamikia kitu

Mashabiki wa Barcelona wakishangilia baada ya kuchukua ushindi wa pili katika bonanza hilo

BAADA YA KULWA(YANGA) KUPIGWA 2-0: DOTO(SIMBA) NAE LEO ANYOLEWA 2-0 NA URA

 

 Derrick Walulya mchezaji wa timu ya URA FC kutoka nchini Uganda ambaye aliwahi kuchezea timu ya Simba pia ya Tanzania akimiliki mpira mbele ya Felix Sunzu mshabuliaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kuwania kombe la Kagame linaloandaliwa na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika Mashariki CECAFA unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni hii mpaka sasa mpira umekwisha na timu ya URA imeifunga timu ya Simba magoli 2-0. magoli hayo yamefungwa na mchezaji Feni Ali wa URA FC.
 Waamuzi wakiongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
 Watangazaji wa kituo cha televisheni cha Supersport cha Afrika Kusini wakitoa tathmini ya mchezo huo kabla ya timu hizo kukutana ambapo inaonyesha kuwa Simba mara nyingi imekuwa ikifungwa na URA FC wakati timu hizo zinapokutana katika michuano mbalimbali.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika katika uwanja wa Taifa kujionea timu yao ikicheza na Waganda URA FC. (Picha kwa hisani ya fullshangwe.blogspot.com)

YUSUPH MANJI NDIO BOSI MPYA WA YANGA - ASHINDA KWA ASILIMIA 97. SANGA MSAIDIZI WAKE.

Kwa mujibu wa tovuti ya klabu ya Yanga haya ndio matokeo kamili ya wagombea ni:

Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji (kura 1876)  97.0%,  John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%, Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%

Nafasi ya Ujumbe: 
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068), Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)

kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama

Monday, July 9, 2012

ROBO FAINALI COPA COCA-COLA 2012

 

Robo Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayokutanisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 inaanza kesho (Julai 10 mwaka huu) kwa timu nne kuumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salam.
 
Temeke na Mjini Magharibi ndizo zitakazocheza robo fainali ya kwanza kuanzia saa 2.30 asubuhi. Mara iliyoivua ubingwa Kigoma itacheza robo fainali ya pili dhidi ya Morogoro kwenye uwanja huo huo.

Robo Fainali ya tatu itachezwa keshokutwa (Julai 11 mwaka huu) kwa kuzikutanisha timu za Kinondoni na Mwanza. Mechi hiyo itaanza saa 2.30 asubuhi na kufuatiwa na nyingine kati ya Dodoma na Tanga itakayoanza 10 kamili jioni.
 
Nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Juni 24 mwaka huu katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikishirikisha timu 28 itafanyika Julai 13 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
 
Mshindi wa mechi kati ya Temeke na Mjini Magharibi, na Kinondoni dhidi ya Mwanza ndiyo watakaocheza nusu fainali ya kwanza. Nusu fainali ya pili itakuwa mshindi wa mechi ya Mara na Morogoro dhidi ya mshindi wa mechi ya Dodoma na Tanga.
 
Fainali itafanyika Jumapili (Julai 15 mwaka huu). Mechi zote kuanzia hatua ya robo fainali hadi fainali zitafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MARINE, TRL NA TPA MWANZA

 

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba ,katikati akishuka kutoka katika meli ya Mv Victoria, mbele ni Kaimu Meneja wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Projest Samson Kaija na nyuma ya Wasziri ni mkjuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga ‘Mtumishi wa Mungu.Tizeba alikuwa katika ziara ya siku moja akitembelea na kupata changamoto za watumishi wa kampuni za Reli (TRL), Huduma za Meli (MSCL) na Mamlaka ya Bandari (TPA) Mwanza .
PICHA NA MASHAKA BARTAZAR WA FULLSHANGWE-MWANZA


 Naibu wa Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba akiongozwa na Kaimu Meneja wa Huduma za Meli (MSCL) Projest Samson Kaija, katikati.Kulia ni Meneja wa TPA Mwanza, Johnston Mutalemwa, kwenda kukagua hali ya meli ya Mv Victoria iliyokuwa imeegeshwa gatini baada ya safari ya Bukoba juzi.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba wa pili kushoto, akielezwa jambo na  kaimu Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya reli (TRL), Kipallo Kisamfu wa kwanza kushoto, katikati mwenye shati jeupe ni DC wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, wa kwanza kulia ni Meneja Mamlaka ya Bandari (TPA) Johnston Mutalemwa, akifuatiwa na Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa vyombo vya majini na nchi kavu (SUMATRA) Alfred Waryana
Kaimu Meneja wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Projest Samson Kaija , Kushoto wakimtembeza Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba ndani ya meli ya Mv Victoria , ili kujionea hali ya meli hiyo ilivyo mbapo aliagiza ifanyiwe ukarabati wa viti vya abiuiria ili kuwaezesha kusafiri kwa raha badala kuona kuwa usafiri wa meli hiyo ni karaha na wa shida.
Mmoja wa wachuuzi wa ndizi,ambaye hakutaka kutaja jina lake, akisubiri usafiri wa kusafirisha bidhaa hiyo kutoka bandari ya Mwanza kaskazini kwenda sokoni baada ya kupakuliwa kutoka ndani ya meli ya Mv Victoria juzi , kutoka mkoani Kagera.

Dkt Charles Tizeba, akizungumza na watumishi wa reli , mamlaka ya bandari na kampuni ya huduma za meli Mwanza, juzi katika ziara yake ya siku moja ili kujionea utendaji wa kamuni hizo za umma.

Tuesday, July 3, 2012

WANAFUNZI SHULE YA MSINGI LUGALO JIJINI DAR-ES-SALAAM WATEMBELEA BUNGENI DODOMA

.

Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la saba wa Shule ya Msingi ya Lugalo Jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao, nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, wakati walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge, wakiwa katika ziara yao ya Kimasomo.







Miongoni mwa wanafunzi hawa, wapo Walimu, Mawaziri, Makatibu, Madaktari, Wabunge na Viongozi mbalimbali wa miaka ijayo, endapo watapewa misingi ya elimu iliyo bora na kupewa elimu ya Nidhamu na utiifu wakiwa bado wadogo, ili waje kuwa viongozi bora siku za baadaye

MILOVAN AONGEZA MKATABA NA SIMBA


.


Kocha mserbia Milovan Cirkovic amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuifundisha Simba, zoezi hilo lilisimamiwa na mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh Ismail Aden Rage.

GAEL CLICHY AMJIBU BALOTELLI - MKEWE NAE MJAMZITO.

Baada ya Mario Balotelli kutangaza kwamba anatarajia kupata mtoto na demu wake Raffaella, leo Gael Glichy amejitokeza mitaani na mkewe wake Charlene Guric ambaye sasa imegundulika ni mjamzito wa miezi minne.

Clichy na mkewe Charlene walionekana wakitembea kwenye maduka ya St.Lopez wakifanya manunuzi ya vitu mbalimbali siku mbili baada ya mchezaji mwenzie wa Manchester City Mario Balotelli na mchumba Modo Raffaella kutangaza kwamba wanatarajia kupata mtoto.



Inaonekana wachezaji wa City wamepania kutengeneza timu nyingine ya watoto wao sasa.

Warsha ya watu wenye ulemavu kuhusu hali ya utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa

 

Mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa Asasi za Kiraia Foundation for Civil Society. Bw. John Ulanga akiongea na washiriki wa mkutano huo juu ya ushiriki wa walemavu katika mchakato wa katiba nchini Mkutano uliandaliwa na Asasi za kiraia za  watu wenye ulemavu nchini chini ya ufadhili wa The Foundation for Civil Society.uliofanyika katika Hotel ya Umbungo Plaza leo jijini Dar es salaam.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
Mkurugenzi wa Haki za Bianadamu kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora nchini, Bw;Francis Nzuki akiongea na washiriki juu ya kazi za tume na wajibu wake kwa jamii ya watu wenye ulemavu nchini.

Mmoja wa washiriki kutoka chama cha walemavu wa ngozi nchini akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo katika washa hiyo.
Mwanasheria na mmoja wa waliofanya utafiti kuhusu hali ya utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa fursa na haki kwa watu wenye ulamvau na sheria zilizopo nchini Bw;Crarence Kipobotoca akiwasilisha utafiti kwa washiriki hao.

Baadhi ya washiriki walioudhuria  mkutano huo wa siku tatu unaoendelea Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam

MABONDIA WA TANGA WAMKUMBUKA BONDIA MAREHEMU MAGOMA SHABANI NA KUMCHANGIA KWA KUTUPIANA MASUMBWI

 

 Bondia Ramadhani Mbwana kushoto akipambana na Patrick Kimweri wakati wa mchezo wa masumbwi uliofanyika Mkoa wa Tanga jana kwa ajili ya kumuenzi na kumchangia bondia Marehemu Magoma Shabani aliefariki Dunia Kimweri alishinda mchezo huo kwa pointi
 MABONDIA  Patrick Kimweri na ramadhani mbwana wakioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi wakati wa mpambano wa kumkumbuka na kumchangia bondia Magoma Shabani Aliefariki Dunia Picha na www.superdboxingcoacvh.blogspot.com
Bondia Yusufu Ally kushoto na Adam Yusufu wakioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi wakati wa mchezo huo kwa ajili ya kumkumbuka na kuchangia Bondia Magoma Shabani alifariki Dunia hivi karibuni Mkoa wa Tanga Adamu Yusufu alishinda kwa Point mchezo

Kazi ya Kukusanya Maoni Kupitia Mikutano Imeanza Vizuri.



 Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Makunduchi Aziza Mcha, akikabidhi barua yake yenye maoni yake kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa kutowa maoni ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania Mohammed Yussuf Mshamba, wakati tume hiyo ilipofika katika Wilaya ya Kusini Unguja kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Katiba, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Mtende.
 Mwananchi wa Kijiji cha Mzuri Makunduchi Duli Ali Duli, akichangia maoni yake kwa Tume iliofika kukusanya maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania, amesema kuwe na Serikali mbili ya Zanzibar na Tanganyika, na kuondoa kasoro zilioko katika Muungano huu.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Balozi Salim Ahmed Salim, akizungumza kuhusiana na utoaji wa maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Mtende

Tuesday, June 26, 2012

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) yatoa msaada katika skuli ya Chokocho mkoani Pemba.

 

 Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Chokocho Idrisa Daudi Ame (Kushoto) akipokea
mfuko wa saruji kutoka kwa mkuu wa Kanda ya Zanzibar inayohusiha mikoa
ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu kama ishara ya kupokea vifaa hivyo.
Kulia ni meneja wa TTCL Pemba Bw. Alphonce Gakwavu.

 Mkuu wa Biashara kanda ya Zanzibar bw. Hussein Nguvu (Kulia)
akimkabidhi sehemu ya Nondo Mwalimu mkuu wa Skuli ya Chokocho Idrisa
Daudi Ame
 Mkuu wa Biashara kanda ya Zanzibar Bw. Husssein Nguvu akimkabidhi simu
za mkononi Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani-Pemba Muhidin Juma Mohamed.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Polisi Jamii Jondeni Sheha M. Sheha

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mifuko ya saruji, nondo pamoja na mchanga katika skuli ya Chokocho mkoani Pemba.

Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Biashara wa Kanda ya Zanzibar inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara Bw. Hussein Nguvu amesema, TTCL ina vipaumbele vingi lakini wameamua kuchangia katika shule kwani wanatambua Elimu ni Mlima, kadri unavyozidi kupanda, ndivyo unavyozidi kuona mbali.

Naye mwalimu mkuu wa skuli ya Chokocho Bw. Idrisa Daudi Ame amesema, wanashukuru sana kwa msaada huo kwani utaleta ahueni katika shule hiyo iliyo na changamoto nyingi ikiwamo uchakavu kwani ilianzishwa miaka mingi iliyopita.

Wakati huo huo, Mkuu huyo wa kanda ya Zanzibar Bw. Hussein Nguvu amekabidhi Vifaa mbali mbali ikiwa ni pamoja na simu za mkononi, viatu vya tope (gum boots) makoti ya mvua (rain coats), vizibao (Reflective jackets) tochi pamoja na filimbi kwa Polisi Jamii Jondeni mjini Pemba.

Akiongea wakati wa kupokea vifaa hivyo Mkuu wa polisi wa Wilaya Mkoani Pemba Muhidin Juma Mohamed ameishukuru kampuni ya TTCL kwa kushirikiana na Jeshi la polisi na hasa Polisi jamii, kwani ulinzi unaenda sambamba na mawasiliano, hivyo simu hizo na vifaa vingine vitawasaidia sana kiutendaji.

Naye mwenyekiti wa Polisi jamii Jondeni Bw. Sheha M. Shaha amesema, anaishukuru TTCL kwa msaada huo kwani utawaongezea ufanisi katika utendaji wa kazi pia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwa karibu na jamii na hasa kiutendaji, na ndio maana wamefanikiwa kufika hapo walipo na wanaweza kufanya kazi kiufanisi bila shuruti.